Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020
|
2015 ←
|
28 Oktoba 2020 (2020-10-28)
|
→ 2025
|
|
|
|
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020 ulifanyika tarehe 28 Oktoba. Wapiga kura walimchagua Rais, wabunge na Madiwani.[1]
Matokeo ya Uchaguzi wa Rais
Kufuatana na tangazo la Tume la Uchaguzi la 30 Oktoba matokeo yalikuwa kama yafuatayo[2]:
Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 29,754,699. Waliopiga kura walikuwa 15,091,950 (% 50.72), wasiopiga kura walikuwa 14,662,749 (% 49.28).
Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 15,091,950. Kura 261,755 ziliharibika. Jumla ya kura halali ilikuwa 14,830,195.
- Magufuli alipata kura 12,516,252 (sawa na % 84.40 za kura halali)
- Lissu alipata kura 1,933,271 (sawa na % 13.04 za kura halali)
- Wagombea wengine kwa jumla walipata kura 380,672 (sawa na % 2.57 za kura halali)
Wagombea Urais
Yaliyofuata
Baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kumaliza kutangaza matokeo, vyama vikuu vya upinzani viliungana kukataa matokeo hayo na kudai uchaguzi huru na wa haki chini ya tume huru vikataja kasoro nyingi za mchakato mzima wa uchaguzi[4]
[5] [6]
Upande wake Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) ulizuia mitandao ya kijamii mbalimbali ili kupunguza mawasiliano hasa kutokana na mauaji yaliyotokea Zanzibar.[5]
Nchi na taasisi mbalimbali zimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu uchaguzi na matokeo yake [7],
[8],
[9][10].
Tarehe 10 Novemba 2020, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki za Binadamu alitoa tamko kuhusu hali tete ya nchi[11] ambalo lilijibiwa mapema na serikali ya Tanzania[12].
Uchaguzi wa 2020 huhesabiwa kuwa ndiyo mbaya kupita yote. Uligubikwa na hila na mbinu chafu. Mbowe alitoa rai yake juu ya uchaguzi huo kwa kusema, ''Kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''[13]
Marejeo