Sinkopu, ambayo pia hujulikana kama kupoteza fahamu au kuishiwa na pumzi, hufasiliwa kama upotezaji mfupi wa fahamu na nguvu za misuli, unaoanyeshwa kwa mwanzo wa haraka, wa muda mfupi wa upataji tena fahamu. Hutokana na kupungua kwa mtiririko wa katika ubongo kutokana na shikizo la chini la damu. Visababishi vingine vina dalili za onyo kabla ya upoteaji wa fahamu kutendeka. Dalili hizi zinaweza kuwa wepesi wa kichwa, kutokwa na jasho, ngozi iliyokwajuka, kutoona vizuri, kutaka kutapika, kutapika, na kujihisi moto miongoni mwa zingine. Sinkopu inaweza pia kuhusishwa na kipindi kifupi cha mshtuko wa misuli. Mtu asipopoteza fahamu na nguvu za misuli kikamilifu, huitwa kitanguliza sinkopu. Imependekezwa kuwa kitanguliza sinkopu kishughulikiwe kwa njia sawa na sinkopu.[1]
Kisababishi
Visababishi ni kutoka kwa visivyo hatari hadi vinavyoweza kusababisha kifo Kuna kategoria tatu pana za visababishi: vinavyohusiana na moyo au mshipa wa damu, rifleksi ambayo pia hujulikana kama inayotokana na neva, na hipotensheni ya wima. Masuala yanayohusiana na moyo na mishipa ya damu ndiyo kisababishi cha takribani asilimia 10 na ambacho ndicho hatari sana ilhali inayotokana na neva ndiyo inayotokea sana. Visababishi vinavyotokana na moyo vinaweza kuwa ridhimu isiyo ya kawaida ya moyo, matatizo ya vali za moyo au misuli ya moyo na kufungana kwa mishipa ya damu kutokana na uemboli wa mishipa au uchanguaji wa mshipa wa aota miongoni mwa mengine. Sinkopu inayotokana na neva hutokea mishipa ya damu inapotanuka na upunguaji wa kasi ya mdundo wa moyo isivyofaa. Hii inaweza kutokana na tukio la kuchochea kama vile kutangamana na damu, maumivu au hisia nzito au shughuli maalum kama vile kukojoa, kutapika, au kukohoa. Aina hii ya sinkopu inaweza pia kutokea sehemu kwenye shingo iitwayo sinasi ya karotidi inapofinywa. Aina ya mwisho ya sinkopu hutokana na kupungua kwa shinikizo la damu kutokana na kusimama wima. Hii hutokana na dawa ambazo mtu anatumia lakini pia inaweza kuhusiana na kuishiwa na maji mwilini, kuvuja damu nyingi au maambukizi.[1]
Sinkopu huathiri takribani watu watatu hadi sita kwa kila watu elfu moja kila mwaka.[1] Hutokea sana kwa wazee na wanawake. Ndiyo sababu ya asilimia moja hadi tatu ya safari kwa vitengo vya dharura na kulazwa hospitalini. Hadi nusu ya wanawake zaidi ya umri wa miaka 80 na thuluthi moja ya wanafunzi wa udaktari huelezea angalau tukio moja maishani mwao.[2] Kwa wote walio na sinkopu, takribani asilimia 4 hufariki kwa siku 30 zinazofuata.[1] Hatari ya matokeo mabaya, hata hivyo, hulingana na kisababishi halisi.[3]
↑Kenny, RA; Bhangu, J; King-Kallimanis, BL (2013). "Epidemiology of syncope/collapse in younger and older Western patient populations". Progress in cardiovascular diseases. 55 (4): 357–63. PMID23472771.
↑Ruwald, MH (Agosti 2013). "Epidemiological studies on syncope--a register based approach". Danish medical journal. 60 (8): B4702. PMID24063058.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!