Shule ya St Jude

St Jude muonekano kwa mbele ya geti
Wanafunzi wa St Jude kwenye assembly
mwanafunzi akiwa shule ya St Jude Arusha, Tanzania
Chai ya Asubuhi shule ya msingi St Jude 03.02.2014 10
Ujumla 28.01.2014 21
Wanafunzi madarasani
Asembly shule ya secondary ya St Jude 30.01.2014 6

St Jude ni shule inayofadhiliwa na ya hisani iliyopo kaskazini mwa jiji la Arusha, Tanzania. Shule hiyo, ambayo ina kampasi tatu, hutoa bure elimu ya msingi na sekondari kwa watoto wasio na uwezo wa Mkoa wa Arusha. Pia hutoa huduma ya bweni kwa zaidi ya wanafunzi 1000 na inaajiri zaidi ya wafanyakazi 270 kitanzania. Ilianzishwa na muaustralia Gemma Sisia mnamo 2002, katika msingi wa imani kwamba elimu ndiyo njia bora ya kupambana na umaskini.[1]

Historia

Shule hiyo ilianzishwa mnamo 2002 na muAustralia Gemma Sisia, ambaye alikuwa na ndoto ya kusaidia kumaliza umasikini barani Afrika. Alithibitisha kuwa mfadhili mwenye talanta kwa kushirikisha watu na mashirika kama Rotary.[2] Aliita shule hiyo baada ya St Jude; mtakatifu mlinzi kwa sababu za kutokuwa na tumaini.[3] 'Mchango wangu wa kwanza ulikuwa $ 10 na sikuwa na uzoefu wa ujenzi kabla ya kuhamia Afrika, kwa hivyo uwezekano wa shule hiyo kupata msingi ulikuwa hauna matumaini! Kwa hivyo, niliamini kuwa kwa bidii, shauku na maombi unaweza kupitia chochote. Hata leo naamini hivyo.'[4]

Shule hiyo hutoa elimu ya bure na ya hali ya juu kwa wasichana na wavulana zaidi ya 1,800 kutoka katika familia zenye uwezo mdogo wa kiuchumi. Ni ufadhili wa asilimia 100[5] na haipati msaada wa serikali kutoka Tanzania au Australia.[6] 90% ya ufadhili wa shule hiyo ni kutoka kwa familia za kawaida za Australia ambao wamejiandikisha kudhamini mtoto au kuchangia.[7]

Asilimia 90 ya ufadhili wa shule hiyo ni kutoka kwa familia za kawaida kutokea Australia ambao wamejiandikisha kudhamini mtoto au kuchangia. Kila mwaka shule hufungua milango yake kuchagua wanafunzi wapya 150 ambao wanaonyesha ahadi za kitaalamu pamoja na hitaji la kweli la fedha. Wasichana na wavulana hawa hupewa kila kitu wanachohitaji kufanikiwa; kutoka elimu ya kiwango cha kimataifa na pia malazi salama na milo mitatu yenye lishe kwa siku.

Mnamo mwaka 2015 darasa la kwanza la wahitimu wa shule hiyo, kidato cha 6, lilimaliza kati ya shule 10 bora nchini Tanzania.[8] Wengi wao walikamilisha mwaka wa Huduma kwa Jamii wakati wakiendelea na maombi ya vyuo vikuu, na Oktoba 2016 walikubaliwa katika Vyuo Vikuu vya juu nchini Tanzania.[9] Hii ni pamoja na wanafunzi 16 ambao wameanza kusoma Udaktari wa Tiba au shahada nyingine zinazohusiana na afya.[10] Hii ni moja wapo ya masomo ya kipaumbele ya kitaifa ya Serikali ya Tanzania pamoja na Kilimo, elimu, Utalii, Uhandisi na IT, yote ambayo yanachukuliwa shahada katika vyuo vikuu na darasa la wahitimu wa shule ya St Jude's wa 2015.[11]

Dhamira

Dhamira ya shule hiyo ni kuelimisha wanafunzi wenye weledi lakini hukosa uwezo wa kusoma kutoka mkoa wa Arusha ili wawe viongozi wenye maadili na wasomi. Wahitimu kutoka St Jude's wanategemewa kuwa wenye heshima, uwajibikaji, waaminifu na wenye fadhili, waajiriwa wanaokidhi viwango, wenye uwezo wa uongozi wa kuaminika katika jamii zao na kwa kiwango cha kitaifa[12]

Lengo kuu la shule ni kupigana na umaskini kwa kupitia elimu na kuchangia katika uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji kote Tanzania.[13]

Miundombinu

Shule ina kampasi tatu. Kampasi ya shule ya msingi, kituo cha wageni na ofisi za utawala zipo Moshono jirani na Arusha mjini. Mabweni ya shule ya msingi kuanzia darasa la tano mpaka la saba yapo umbali wa dakika kumi na tano (mda wa matembezi) katika eneo la Moivaro. Kampasi ya sekondari inajumuisha mabweni yake yenyewe na shamba la ukubwa wa ekari 6, kampasi hii ipo katika mji mdogo wa Usa River, umbali wa dakika ishirini (mwendo wa gari) kutoka kampasi ya msingi au Arusha mjini.

Shule hii inamiliki mabasi ya shule 27 ambayo inahakikisha wanafunzi wanafika shuleni kwa usalama kutoka nyumbani kwao. Nyumba mbili za maktaba zenye zaidi ya vitabu elfu thelathini, CD na DVD. Wanafunzi wanapata maabara ya sayansi, uwanja wa michezo, na vyumba vya kompyuta na sanaa. Wanafunzi wote hunywa chai asubuhi na chakula cha mchana kila siku. Wanafunzi wa bweni pia hupokea kifungua kinywa na chakula cha jioni. Shule hiyo hutoa wastani wa milo milioni kwa mwaka. Shule hiyo imeajiri zaidi ya wafanyakazi 270 wa Afrika Mashariki na zaidi ya watu 15 wa kujitolea wa kimataifa kutoka ulimwenguni kote.[14]

Elimu kwa wasichana

Wasichana hufanya zaidi ya nusu ya idadi ya wanafunzi wa shule hiyo na asilimia hii ilifikiwa bila matumizi ya upendeleo. Shule inafuata vigezo viwili tu katika uchaguzi wa wanafunzi: talanta ya kitaaluma na hitaji la kweli la kifedha.

Nchini Tanzania ni kawaida kwa watoto wa shule, bila kujali jinsia, kukata nywele zao na muda wotye wakati wa shule ziwe fupi na nadhifu. Kuangalia picha za wanafunzi wadogo wa St Jude, inaweza kuwa ngumu kutambua jinsia zao.

Mnamo 2013, Gemma Sisia alielezea sera yake ya kijinsia katika chapisho la blogi[15] kwenye wavuti ya shule. Mtazamo wake ni kwamba kuingiza ubora katika mifumo ya elimu, haswa kusini mwa jangwa la sahara, ni jambo muhimu linalokosekana kwa mjadala wa elimu ya wasichana.

Rotary Australia

Sisia alijua atalazimika kutafuta pesa nyingi inayofaa kujenga shule ya ndoto zake. Ilikuwa ni baba yake ambaye alikuwa na wazo. Kwa ushauri wake, aliwasiliana na vilabu vya karibu vya karibu na familia yake. Gemma na rafiki wa familia, David Steller, walipiga simu kwa watu mbalimbali na kwa muda mfupi washirika na wanachama wa vilabu vya Rotary huko Australia, walianza kuleta shule za mitaani kwao.

Waliweka meza katika duka la ununuzi ambapo wafanyakazi wa kujitolea walibadilishana zamu kuuza matofali ya karatasi kwa $2 yanayowakilisha kazi za ujenzi ambazo zilihitaji ufadhili. Katika miezi michache, waliweza kutengeneza pesa zilizohitajika. Ndivyo ilianza ushirikiano wa muda mrefu kati ya shule ya St Jude and Rotary.

Hadithi ya kusisimua ya Gemma na sifa yake kama msemaji anayependwa na mwenye kujishughulisha ilisababisha apate mialiko mingi ya kuongea kwenye Vilabu vya Rotary. Kuanzia wakati huo, idadi ya watu, vilabu vya mzunguko, shule, taasisi, makanisa na biashara yenye nia ya kusaidia viliongezeka mfano wa theluji inapo poromoka mlimani. Mnamo mwaka 2000, wakati ulipofika wa kujenga shule, Armidale Central Rotary Club ilipanga kikundi cha kujitolea chenye idadi ya watu 13 kusafiri kwenda Tanzania na kujenga jengo la kwanza la vyumba vya madarasa. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa timu nyingi za kujitolea za Rotari kujihusika na shule ya St Jude. Wanachama wa rotary ambao walibaki Australia walisaidia katika ukusanyaji na usafirishaji wa kompyuta, vitabu vya maktaba na vitabu vya shule, vifaa vya kufundishia, vifaa vya darasani, vifaa vya michezo, mashine za kushona, nguo na orodha isiyo na mwisho ya bidhaa. Wanachama wengi wa rotary hutembelea St Jude kila mwaka.

Mnamo mwaka 2016, wanafunzi waandamizi wa St Jude walianzisha tawi lao la Rotary kwa vijana.ref>[2] Ilihifadhiwa 5 Mei 2016 kwenye Wayback Machine..</ref>

Msaada wa Kimarekani na Hali ya Hisani

Kampasi ya sekondari imepewa jina la Smith kama ishara ya heshma na shukrani kwa familia iliopo Marekani katika jiji la Washington, D.C ya Gordon V. na Helen C. Smith Foundation. Uhusiano wao na St Jude ulitokea baada ya familia kusafiri kwa pamoja kwenda Tanzania mnamo mwaka 2004 na mwongoza matembezi aliwapeleka kutembelea shule moja ya umma. Wa-Smith wana historia ndefu ya kusaidia mipango ya kielimu. Baada ya kuona madarasa yenye wanafunzi hadi 120 na rasilimali chache, waliamua kuunga mkono mpango wa misaada unaolenga fursa za elimu nchini Tanzania. Miezi michache baadaye, wanafamilia walirudi Arusha, walitembelea shule kadhaa na waliamua kujihusisha na St Jude. Mchango wao na ushiriki wa kibinafsi ulifanya iwezekane kwa St Jude's kupanua toleo lake la elimu kufikia kiwango cha shule za sekondari.

Mnamo Septemba 2016 shule ilitangaza kuwa Marafiki wa Amerika wa Shule ya St Jude, Tanzania, Inc. walizindua tovuti mpya; https://www.afstjude.org/ Ilihifadhiwa 15 Januari 2021 kwenye Wayback Machine., Jalada la kugharamia ufadhili la St Jude Marekani linatambuliwa rasmi kama shirika la misaada ya umma 501 (c) (3) na shirika la Marafiki la Amerika limepewa dhamana rasmi ya ushuru wa kodi EIN 47-3077055. Hii inaruhusu wafuasi wa Marekani kutoa kwa St Jude michango rahisi, isiyotozwa ushuru na uhakikisho kwamba michango yoyote ya kifedha inatekelezwa kwa kiwango kamili kwa mujibu wa sheria.

Wageni na Maneno ya kinywa

Kama sehemu ya shughuli zake za kutafuta fedha na kujitangaza, shule hupokea mamia ya wageni kila mwaka kwa ziara za siku za maeneo ya shule. Wadhamini wa wanafunzi wanahimizwa kutembelea shule na wanaweza kushiriki katika ziara za nyumbani kuona familia za wanafunzi. Hadi wageni 60 wanaweza kukaa katika makao bora ya mtindo wa hoteli ambayo yana bafuni za ndani, net kuzuia mbu na jiko la wageni lililo na vifaa kamili vya upishi. Timu ya wageni iko kila siku na inaweza kuandaa mpango wa shughuli ikiwa inahitajika.

Wageni ni sehemu muhimu ya kampeni ya shule ya kuhamasisha wageni, wafadhili na wadhamini wenye uwezo wa kusaidia shule mawasiliano ya kinywa. Shule ya St Jude pia inatoa ziara maalum za wiki mbili au tatu pamoja na safari katika mbuga za kitaifa za Serengeti na Ngorongoro, safari za kuona makabila na safari kwenda Zanzibar.

Gemma Sisia

Gemma Sisia (née Rice) alizaliwa mnamo Novemba 3, 1971. Alitumia miaka yake utotoni kwenye ufugaji wa kondoo wa pamba nje kidogo ya Guyra huko kaskazini mwa New South Wales, Australia. Kama binti wa pekee kati ya watoto nane wa Sue na Basil Rice, Gemma alilazimika kwenda na ndugu zake wakati wa kufyatua kondoo na kuendesha farasi. Mama yake Gemma, Sue, anaamini hili ambapo msimamo wa binti yake Gemma ulitokea; "Sidhani kama unaweza kumshawishi Gemma kufanya ama kuacha kitu chochote."[16] Sue Rice bado anaishi katika eneo la familia huko Guyra na ndugu zake kadhaa. Basil, baba yake Gemma, alifariki mnamo mwaka 2004.[17]

Baada ya kuhitimu masomo ya sekondari katika Chuo cha St Vincent's huko Sydney.,[18] Gemma aliamua kusoma Shahada ya Sayansi Chuo Kikuu. Alijikita katika genetics na Biochemistry huko Chuo Kikuu cha Melbourne[19] and the University of Northern Territory ambapo alipata shahada daraja la Kwanza. Gemma alimaliza masomo yake ya juu na diploma ya elimu kupitia Chuo Kikuu cha New England (Australia) University of New England.

Akiwa na umri wa miaka 22 na shauku na bidii aliyerithi kutoka kwa baba yake, Edmund Rice (mwanzilishi wa harakati ya Christian Brothers), Gemma alitumia wakati fulani kusaidia watu wasio na uwezo wa kifedha barani Afrika. Alisafiri kwenda Uganda, Afrika Mashariki na kufanya kazi kwa miaka mitatu kama mwalimu wa kujitolea. Uzoefu huu ulisababisha imani ya dhati kwamba elimu ya bure na ya hali ya juu inapaswa kuwa haki ya watoto wote ulimwenguni, na kwamba elimu ndio silaha kali katika vita dhidi ya umaskini, rushwa na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa.

Aliporudi kwao Australia, Gemma alianza kukusanya pesa ya kufadhili na kusaidia watoto wanyonge nchini Uganda ili kumaliza shule. Akifurahishwa na msaada na michango, Gemma alifanikiwa kutengeneza pesa nyingi, za kutosha hivi kwamba alianzisha mfuko rasmi kuwekeza katika elimu ya watoto wasio na uwezo wa kifedha Afrika Mashariki. Baada ya kugundua kuwa fedha alizotoa kama msaada hazikuwa zikisambazwa vizuri, aliamua kurudi Afrika Mashariki kusimamia pesa hizo mwenyewe.

Akiwa aanafanya kazi nchini Uganda Gemma alienda likizo nchi jirani ya Tanzania. Ilikuwa ni safarini alipokutana na kupendana na Richard Sisia, aliekua dereva wa safari yake, ambaye walipanga baadaye aje kuwa mume wake.[20] Mnamo mwaka1998 Daniel Sisia, baba mzazi wa Richard na baba mkwe wa Gemma, alimpatia Gemma shamba ndogo huko Arusha ili kujenga shule ya kusadia watoto wasio na uwezo wa kifedha kwenda shule.[21] Gemma alianza kujenga Shule ya St Jude kwenye ardhi hii na dhamira ya kusaidia watoto wasio na uwezo wa kifedha kupata elimu. Shule hiyo ilifunguliwa mnamo mwaka 2002 ikiwa wanafunzi watatu waliodhaminiwa na imekua mfululizo tangu hapo.

Mnamo mwaka 2000, Gemma alipewa tuzo ya Sapphire Paul Harris Fellow na Rotary International..[22] Autobiografia ya Gemma, St Jude's , ilichapishwa na Pan Macmillan Australia mnamo 2007 na ilibaki kwenye orodha ya mauzo bora kwa zaidi ya miezi miwili. Pia mnamo mwaka 2007, mafanikio ya Gemma yalitunukiwa kwa Agizo la medali ya Australia..[23] Hadithi ya Gemma imeonyeshwa mara mbili katika programu ya maandishi ya runinga ya ABC Hadithi ya Australia mwaka 2005 na 2009. Mnamo mwaka 2012, Gemma alitajwa katika bodi ya Mapitio ya Fedha ya Australia The Australian Financial Review na Westpac's 100 Women of Influence kama mmoja wa na Wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. Alishinda pia katika shindano la muaustralia wa mwaka huko New South Wales.

Miaka muhimu

1998

  • Daniel Sisia awapa Gemma na Richard ekari mbili za ardhi kwaajili ya kujenga shule.
  • Gemma anapokea msaada wa kwanza wa $10 AUD(dola ya Australia) kutoka kwa Agnes Hanna ili kuanza harakati za kutafuta fedha.

2000

  • Klabu ya Rotary ya Armidale Central inajenga chumba cha kwanza cha darasa.

2001

  • Gemma aifanya Tanzania 'nyumbani'.

2002

  • St Jude inafunguliwa mnamo Januari 29 ikiwa na wanafunzi watatu na mwalimu mmoja, Angela Bailey.
  • Bodi ya Shule na Kamati ya Wazazi inaundwa.
  • Rotary Australia inatoa makato ya ushuru, shukrani kwa Monica Hart na Jack Elliot.

2003

  • St Jude inasomesha wanafunzi 120 na inaajiri wafanyikazi 23 wa kitanzania.
  • Nyumba ya wageni (The yelow house) ilijengwa. Wanaojitolea hawakai tena kwenye mahema.

2004

  • St Jude inasomesha wanafunzi 423 na inaajiri zaidi ya wafanyakazi 80 wa kitanzania
  • Maktaba, uwanja wa mpira na vyumba vipya 12 vya madarasa vinajengwa.
  • Idadi ya mabasi inakua hadi 8.
  • Wanafunzi na wafanyikazi sasa wanaweza kufurahia chakula cha mchana.
  • St Jude inaunganisha kwenye mtandao.

2005

  • Gemma anashiriki kwa mara ya kwanza kwenye programu ya runinga ya ABC Television kwa jina la Australian Story[24].
  • Kamati ya wazazi inafikisha jumla ya wajumbe 20.
  • Tovuti ya kwanza ya shule inatengenezwa na muaustralia Richard Pagliaro.
  • Bwalo la Moshono lafunguliwa.
  • Wanafunzi wa kwanza wa darasa la nne wanafanya mtihani wa kitaifa National Exam na kushika nafasi ya tatu kiwilaya.

2006

  • St Jude inasomesha wanafunzi 662 na inaajiri wafanyikazi 114 wa kitanzania.
  • Siku ya utamaduni yafanyika shuleni kwa mara ya kwanza.
  • Ekari 30 za shamba zanunuliwa Usa kwa ajili ya kampasi ya pili.
  • Kwa mara ya kwanza shule inafanya hafla ya kumuenzi Mt Yuda na kuwapa wanafunzi nafasi ya kutoa shukrani.

2007

  • St Jude inasomesha wanafunzi 850 na inaajiri wafanyikazi 127 wa kitanzania.
  • Timu ya kwanza ya ukaguzi wa afya inakuja St Jude's.
  • Gemma anapata tuzo ya heshima kutoka Australia.[25]
  • Australian inazindua kitabu cha Gemma kwa jina la St Jude's.[26]
  • Bweni ya Moivaro yafunguliwa ikiwa na wanafunzi wapatao 300.

2008

  • St Jude inasomesha wanafunzi 989 na inaajiri wafanyikazi 330 wa kitanzania.
  • Kampasi ya shule ya msingi yafunguliwa Usa River ikiwa na wanafunzi wapatao 500,[27] kati yao 250 wanalala bwenini.
  • Darasa la saba wafanya mtihani wa kwanza wa kitaifa na kua kati ya 10% ya shule zilizofanya vizuri nchini. Alex Elifas, mwanafunzi wa St Jude anashika nafasi ya 23 kati ya wanafunzi zaidi ya milioni moja nchi nzima.

2009

  • Kwa mara nyingine Gemma ashirikishwa kwenye historia ya Australia( Australian Story)[28] and speaks at Australia's Parliament House.
  • Kampasi ya sekondari yafunguliwa Moshono ikiwa na wanfunzi 51 wa kidato cha kwanza, kwa mara ya kwanza shule yapokea wanafunzi wahitimu wa darasa la saba kutoka shule za serikali kujiunga na kidato cha kwanza.
  • Wafanyakazi na wanafunzi wapatao 150 washiriki hafla na raisi mstaafu wa wa Tanzania wa awamu ya nne mh.Jakaya Kikwete.
  • Poromoko la Uchumi ulimwenguni latokea: wafanyakazi wapatao 47 wapunguzwa pamoja na punguzo la mshaara kwa 10%.
  • St Jude's ina walimu wakuu watatu.

2010

  • St Jude's inaelimisha wanafunzi wapatao 1,300 (900 kati yao wakiwa bweni), imeajiri wafanyakazi Zaidi ya 340 wa kitanzania na kutoa Zaidi ya milo 772,000 kwa watu wote.
  • Punguzo la mshahara kwa 10% lafikia kikomo.
  • Wanafunzi wa kidato cha pili wafanya mtihani wa kitaifa na kushika nafasi ya 3 kati ya shule 302 – katika ukanda wa kaskazini mashariki.
  • Idadi ya mabasi yakua na kufika 20.

2011

  • Wito wa misaada kwa ajili nya kiwanja kipya cha michezo cha sababisha mapato ya dola 115,000.
  • St Jude inatoa Zaidi ya milo 850,000.

2012

  • Januari 29 shule ya St Jude yaadhimisha jubilei ya miaka 10.
  • Matokeo ya kidato cha nne yaiweka St Jude nafasi ya kwanza katika mkoa wa Arusha nay a saba Tanzania nzima.
  • Bodi ya mapitio ya uchumi Australia pamoja na Westpac wamteua Gemma kama mmoja waa wanawake wenye ushawishi mkubwa '100 Women of Influence'.

2013

  • Felix Mollel awa mfanyakazi wa kwanza wa kitanzania kusafiri nje ya nchi kusambaza taarifa kuhusu St Jude.
  • Matokeo ya kidato cha nne yaiweka St Jude katika nafasi ya tatu kimkoa nay a 20 kitaifa.

2014

  • St Jude's inaelimisha wanafunzi 1,832.
  • Darasa la kwanza la kidato cha sita linaanzishwa na kwa mara ya kwanza St Jude in wanafunzi wa kila darasa. Kwa sasa shule inaelimisha wanafunzi 1,800 na ipo tayari kwa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita mwaka ujao wa 2015.

2015

  • St Jude's inaelimisha wanafunzi 1,899, kati yao 1,389 ni wa bwenini.
  • Takriban 93% kati ya wafanyakazi wetu 339 ni watanzania.
  • Idadi ya mabasi inafikia 27.
  • Mnamo tarehe 30 Mei, kwa furaha kubwa shule inasherehekea mahafali ya kwanza ya kidato cha sita, idadi ya wahitimu ikiwa 61, mahafali yalihudhuriwa na Zaidi ya watu 1000, wazazi na walezi, wageni waalikwa, wafadhili na wageni wengine wa kimataifa.
  • Programu ya ‘Baada ya St Jude(BSJ) inaanza rasmi, wahitimu wa kidato cha sita wakitoa msaada kwa kufundisha Zaidi ya wanafunzi 10,000 kutoka shule 21 za uma.

2016

  • Wanafunzi wapata 131 wanasherehekea mahafali ya pili ya kidato cha sita pamoja na mamia ya walimu, wazani, walezi na wageni waalikwa.
  • St Jude inashiriki kwenye kipindi cha 60 minutes Australia, zilizotazamwa na kaya zaidi ya 800,000 za Australia.
  • Wahitimu wa kwanza wa St Jude's walioshiriki katika mapango baada ya St Jude(BSJ) waanza masomo ya vyuoni, Zaidi ya robo tatu wakichukua masomo ya afya.
  • Mhitimu wa kidato cha sita Dorice Livingstone, awa mwanafunzi wa kwanza kusafiri kwenda Australia na Gemma.
  • St Jude's inaanzisha mfuko wa baadae, lengo likiwa kusisitiza mustakabali wa muda mrefu wa shule.

2017

  • St Jude inapewa uwenyeji wa kuandaa mashindano ya riadha kwa mwaka 2018 maarufu kwa jina la ‘Gold Coast Commonwealth Games Queen's Baton Relay.’
  • Wahitimu 133 wanasherehekea mahafali ya tatu ya kidato cha sita pamoja na mamia ya wazazi, walezi na jamii izungukayo shule.

Tazama pia

Marejeo

  1. The School of St Jude.
  2. "School of St Jude, Arusha, Tanzania". (en-GB) 
  3. "Q & A with Gemma Sisia | About Us | The School of St Jude". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. "Q & A with Gemma Sisia | About Us | The School of St Jude". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  5. "Living The Great Australian Dream... In Africa". Huffington Post Australia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-18. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  6. Cheshire, Ben. "'We call this heaven': Gemma Sisia's Tanzanian story", 2015-11-27. (en-US) 
  7. Cheshire, Ben. "'We call this heaven': Gemma Sisia's Tanzanian story", 2015-11-27. (en-US) 
  8. Bartley, Rachel. "Double the graduates, double the joy at St Jude’s second ever Form 6 graduation!", June 2016. 
  9. "The future's bright!". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  10. "The future's bright!". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  11. "The future's bright!". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  12. "Strategic Plan | About Us | The School of St Jude". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  13. "Strategic Plan | About Us | The School of St Jude". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  14. Verified by the School of St Jude Purchasing, HR and Marketing Teams, written by Angela Stoddard, St Jude's Communications Officer, October 2016.
  15. [1] Ilihifadhiwa 5 Februari 2014 kwenye Wayback Machine..
  16. Cheshire, Ben. "'We call this heaven': Gemma Sisia's Tanzanian story", 2015-11-27. (en-US) 
  17. Cheshire, Ben. "'We call this heaven': Gemma Sisia's Tanzanian story", 2015-11-27. (en-US) 
  18. "Gemma Sisia - The School of St Jude » St Vincent's College". www.stvincents.nsw.edu.au. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-19. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  19. "Ms Gemma Sisia BSc • Events at The University of Melbourne". events.unimelb.edu.au. Iliwekwa mnamo 2016-10-18.
  20. "Q & A with Gemma Sisia | About Us | The School of St Jude". www.schoolofstjude.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  21. "Educating for big dreams and the power of possibility", 2016-10-05. Retrieved on 2019-08-26. Archived from the original on 2017-03-04. 
  22. "Gemma Sisia - The School of St Jude » St Vincent's College". www.stvincents.nsw.edu.au. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-19. Iliwekwa mnamo 2016-10-18. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  23. "How this country girl and St Jude are changing the lives of Tanzania's poorest children | The Catholic Leader". catholicleader.com.au. Iliwekwa mnamo 2016-10-19.
  24. "The School of St Jude", Australian Story, 2005-08-15. 
  25. "Order of Australia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 2019-08-26.
  26. St Jude's
  27. "An international celebration for the school of St Jude at Usa River", The Arusha Times, 2008-07-12. 
  28. "Africa Calling", Australian Story, 2009-06-08. 

Viungo vya nje

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!