Sakhalin (rus. Сахалин) ni kisiwa kikubwa cha Urusi kwenye kaskazini ya Bahari Pasifiki kilichopo kati ya 45°50' na 54°24'. Ni sehemu ya mkoa wa Sakhalin Oblast. Iko karibu na pwani la mashariki la Urusi na karibu na ncha ya kaskazini ya Japani.
Eneo lake ni kilomita za mraba 72,492 kuna wakazi 580,000. Wakati wa karne za 19 na 20 ulikuwa na mavutano kati ya Japani na Urusi kuhusu utawala wa kisiwa. Hadi 1945 kiligawiwa kati ya mataifa haya mawili. urusi ilitwaa kisiwa chote mwaka 1945 baada ya kushinda Japani kwenye Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Wenyeji asilia walikuwa Waaini na wengi wao walihamia Japani baada ya 1945.[1]
Leo hii wakazi wengi kabisa ni Warusi. Takriban 5% ni Wakorea waliohamishwa hapa na serikali ya Urusi kwa kazi kwenye migodi ya makaa mawe.
Usafiri na Urusi bara unapatikana kwa njia ya feri na eropleni.
Uchumi unategemea mafuta ya petroli, gesi asilia, uchimbaji wa makaa mawe, uvunaji wa ubao kwenye misitu na uvuvi. Uzalishaji wa mafuta ya petroli uliongezeka sana tangu mwaka 2000. Makampuni ya ExxonMobil na Shell yalinunua vibali vya kuzalisha gesi na mafuta..