Mji huo uko kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa (huko huitwa Ziwa Malawi) ikiwa ni mojawapo ya bandari kuu kwenye ziwa hilo.
Jiografia
Nkhotakota iko kwenye mwinuko wa mita 472 kwenye mwambao wa Ziwa Malawi. [1] Iko kwenye ukingo wa miamba unaotazamana bandari ya asili iliyoundwa na kisiwa cha mchanga . [1]
Nkhotakota iko umbali wa kilomita 200 kutoka Lilongwe, mji mkuu wa Malawi, na kilomita 378 kutoka Blantyre, jiji kubwa zaidi la Malawi. [2]
MmisionariDavid Livingstone alitembelea mji mara mbili kwenye miaka 1861 na 1864 na kuleta taarifa juu ya ubaya wa biashara ya watumwa hadi Ulaya. Kuna miti miwili inayokumbukwa kama "Livingstone tree" ambako anasemekana alijadiliana na mkuu wa Waarabu Salim bin Abdullah [4]. Baadaye rais wa Malawi Hastings Banda alitoa hotuba chini ya mti mwingine huko Nkhotakota katika miaka ya 1960, huu unaojulikana kama Mti wa Livingstone. [4] Mji huu ulikumbwa na mafuriko ya mwaka 2001, na ulikuwa eneo lililoathiriwa zaidi katika eneo la Kati la Malawi. [5] Leo, Nkhotakota ndio mji mkubwa wa kitamaduni wa Kiafrika nchini Malawi [1] na una ushawishi mkubwa wa Waswahili-Waarabu. [6]
Usafiri
Nkhotakota ni mojawapo ya bandari kuu kwenye Ziwa Nyasa, [7] ikihudumiwa na kivuko cha MV Ilala ambacho huvuka ziwa kila wiki. Uwanja wa ndege wa karibu uko Kasungu kwa umbali wa km 77. Mabasi hutumia masaa 2 kutoka Salima. [8] Aidha, mabasi madogo yanatoka hapa hadi Nkhata Bay kando ya barabara kuu inayounganisha miji hii. [9]
↑"Malawi distance table". Wild Malawi. 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2008. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)