Nchi kavu ni sehemu ya uso wa dunia isiyofunikwa na maji kama sehemu za bahari, maziwa au mito[1]. Nchi kavu inaweza kufunikwa na maji kwa muda katika hali ya mafuriko.
Maisha ya kibinadamu pamoja na kiasi kikubwa cha shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, makazi ya watu na uzalishaji wa bidhaa hutokea kwenye nchi kavu.
Sehemu ambako nchi kavu hukutana na magimba ya maji huitwa pwani au ufuko. Mahali mbalimbali hakuna mstari kamili kati ya nchi kavu na gimba la maji hasa penye kanda la kinamasi au matopetope.
Nchi kavu ni sehemu ya juu ya ganda la dunia lililotokea katika historia ya dunia yetu wakati sehemu za nje ya dunia zilipoanza kupoana na mvuke wa maji ulipopoa na kuwa maji kiowevu. Kuna melezo mawili ya kisayansi kuhusu kutokea kwa nchi kavu[2] yanayosema ama nchi kavu iliongezeka polepole hadi leo[3] au haraka zaidi tangu kale[4] katika historia ya dunia[5] na eneo la nchi kavu halikubadilika kwa muda mrefu.[6][7][8]
Mabara yalipokea maumbo yao kutokana na miendo ya gandunia ambayo ni mchakato unaoendeshwa kwa joto linalopanda juu kutokana na joto la kiini cha dunia. Katika mchakato huo mabara yalitokea na kuvunjika katika kipindi cha miaka mamilioni mara kadhaa. Mabara ya zamani yalikuwa mwanzoni Rodinia, halafu Pannotia, halafu Pangaea iliyovunjika pia takriban miaka milioni 180 iliyopita na kuwa mabara ya leo. [9]
Nchi kavu na halihewa
Kuwepo kwa nchi kavu ni muhimu kwa tabianchi na halihewa hasa katika maeneo ya ufukoni. Halijoto ya nchi kavu hubadilika haraka zaidi kulingana na mnururisho wa jua kuliko uso wa magimba ya maji. Kwahiyo halijoto ya nchi kavu hupanda haraka zaidi wakati wa mchana na kupoa haraka zaidi kuliko uso wa maji wakati wa usiku.
Hivyo kuna tofauti ya halijoto baina nchi kavu na bahari na hii inasababisha kutokea kwa upepo. Hewa joto zaidi inapanda juu na hewa baridi zaidi inachukua mahali pake.
Marejeo
↑Michael Allaby, Chris Park, A Dictionary of Environment and Conservation (2013), page 239, ISBN 0199641668.
↑De Smet, J.; Van Den Berg, A.P.; Vlaar, N.J. (2000). "Early formation and long-term stability of continents resulting from decompression melting in a convecting mantle". Tectonophysics. 322 (1–2): 19. Bibcode:2000Tectp.322...19D. doi:10.1016/S0040-1951(00)00055-X.
↑Kleine, Thorsten; Palme, Herbert; Mezger, Klaus; Halliday, Alex N. (2005-11-24). "Hf-W Chronometry of Lunar Metals and the Age and Early Differentiation of the Moon". Science. 310 (5754): 1671–1674. Bibcode:2005Sci...310.1671K. doi:10.1126/science.1118842. PMID16308422.
↑Hong, D.; Zhang, Jisheng; Wang, Tao; Wang, Shiguang; Xie, Xilin (2004). "Continental crustal growth and the supercontinental cycle: evidence from the Central Asian Orogenic Belt". Journal of Asian Earth Sciences. 23 (5): 799. Bibcode:2004JAESc..23..799H. doi:10.1016/S1367-9120(03)00134-2.