N.W.A

N.W.A
N.W.A (kushoto kwenda kulia): Ice Cube, Dr. Dre, Eazy-E, DJ Yella,MC Ren

N.W.A (kushoto kwenda kulia): Ice Cube, Dr. Dre, Eazy-E, DJ Yella,MC Ren
Maelezo ya awali
Asili yake South Central Los Angeles, Compton, California, Marekani
Aina ya muziki Hip hop
Miaka ya kazi 1986–1991
1999–2000 (Muungano wa Muda)
Studio Ruthless, Priority, EMI
Ame/Wameshirikiana na Above the Law, Bobby Jimmy and the Critters, C.I.A., Fila Fresh Crew, J. J. Fad, Snoop Dogg, The D.O.C., World Class Wreckin' Cru
Wanachama wa sasa
Eazy-E
Dr. Dre
Ice Cube
DJ Yella
MC Ren
Arabian Prince


N.W.A (kifupisho cha Niggaz Wit Attitudes)[1][2][3] lilikuwa kundi la muziki wa hip hop kutoka mjini Compton, California, nchini Marekani. Kundi hili hutazamiwa kama miongoni mwa makundi yaliyochochea mtindo wa gangsta rap,[4] wakati mwingine hutazamiwa tena kama kundi muhimu sana katika historia nzima ya muziki wa hip hop.[5] Lilianza kazi zake tangu mwaka wa 1986 hadi 1991, kundi lilizua minong'ono ya hapa na pale hasa kwa hali halisi ya mashairi yao makali, na hatimaye kufungiwa nyimbo zao zisipigwe katika vituo kadha wa kadha huko nchini Marekani. Licha ya hilo kutokea, kundi liliuza nakala zaidi ya milioni 10 ya CD kwa Marekani pekee. Kutokana na ukatili wa polisi na ukosefu wa usawa wa rangi katika maeneo wanayotokea wanachama wake, kundi hili lilitengeneza muziki wa kisiasa. [6]Wanachama wa kundi hili walionyesha wazi kuchukia mfumo wa polisi, mfumo ambao umezua mijadala mingi kwa miaka mingi.

Kundi linaunganishwa na mtu kama Arabian Prince, DJ Yella, Dr. Dre, Eazy-E, Ice Cube, na MC Ren. Walitoa albamu ya mkusanyiko ya kwanza kama kundi mnamo mwaka 1987, iliitwa N.W.A. and the Posse na ilishika nafasi ya 39 kwenye chati ya Albamu bora za R&B/Hip-Hop inayochapishwa na jarida la Billboard. Arabian Prince alijitoa muda mfupi baada ya kutolewa kwa studio albamu ya kwanza ya N.W.A, Straight Outta Compton, mwaka wa 1988, huku Ice Cube naye akifuata nyayo mnamo Desemba 1989 kwa sababu za mgogoro wa kimaslahi. Wanachama mbalimbali wa kundi hili baadaye wakaja kuuza nakala zilizofikia kiwango cha platinamu katika miaka ya 1990. Albamu ya kwanza ya kundi imenakiliwa kama mwanzo wa zama mpya za Gangsta rap kwani utayarishaji wake na maoni ya kijamii katika mashairi yao yalikuwa mapinduzi makubwa ndani ya mtindo huu.[7] Studio albamu ya pili ya N.W.A, Niggaz4Life, ilifika namba moja kwenye chati za mauzo za Billboard 200.[8]

Rolling Stone iliiorodhesha N.W.A katika nafasi ya 83 kwenye orodha yake ya "Wasanii Wakubwa 100 wa wakati wote". [9]Mnamo mwaka wa 2016, kundi hili liliingizwa kwenye Jumba la Umaarufu la Rock na Roll, baada ya kupendezwa mara tatu hapo awali.

Historia

Nembo ya N.W.A

Kuanzishwa na "Panic Zone" (1987–1988)

Bango la moja ya tamasha la kwanza la N.W.A katika eneo la Compton skating rink, 1988

Kundi la N.W.A lilianzishwa na rapa kutoka Compton, California, Eazy-E. Easy-E alianzisha studio ya kurekodi muziki ya Ruthless Records akiwa na Jerry Heller. Kundi liliunganisha marapa wengine kama Dr. Dre na Ice Cube kisha baadaye akaongezeka DJ Yella na Arabian Prince.[10]

Dre na Yella wote walikuwa wanachama wa zamani wa kundi la World Class Wreckin' Cru kama Ma-DJ na watayarishaji. Studio ya Ruthless ilitoa wimbo wa "Panic Zone" mnamo 1987 kwa kushirikiana na Macola Records, wimbo huu ulijumuishwa kwenye albamu ya mkusanyiko ya N.W.A. and the Posse . N.W.A ilikuwa bado katika hatua zake za mwanzo, na imehusishwa kwenye nyimbo tatu tu kati ya kumi na moja, nyimbo hizo ni pamoja na "Panic Zone", "8-Ball", na "Dopeman", huu ulikuwa ushirikiano wa kwanza wa Arabian Prince, DJ Yella. , Dr. Dre, na Ice Cube. Rapa wa Mexico Krazy-Dee alishiriki kuandika wimbo wa "Panic Zone", ambao awali uliitwa "Hispanic Zone", lakini jina lilibadilishwa baadaye Dr. Dre alipomshauri Krazy-Dee kwamba neno "hispanic" lingepunguza mauzo. Wimbo binafsi wa Eazy-E "Boyz-n-the-Hood" nao ulijumuishwa kwenye hii albamu ya mkusanyiko.[11]

Straight Outta Compton, Eazy-Duz-It (1988–1989)

N.W.A walishiriki kwenye tamasha la ziara ya kundi la Public Enemy 1988 "Bring the Noise".

N.W.A walitoa studio albamu yao ya kwanza, Straight Outta Compton, mwaka wa 1988. Wimbo wa ufunguzi "Straight Outta Compton" ulilitambulisha kundi, "Fuck tha Police" ulipinga ukatili wa polisi na wimbo wa "Gangsta Gangsta" ulitoa mtazamo wa ulimwengu wa vijana wa mjini. Ingawa kundi lilipewa sifa ya kuanzisha tanzu ya muziki ya gangsta rap, N.W.A waliita muziki wao "rap ya kweli". [12]

Dr. Dre na DJ Yella, kama HighPowered Productions, walitayarisha midundo ya kila wimbo, huku Dre akishiriki kama rapa kwenye baadhi ya nyimbo. The D.O.C., Ice Cube, na MC Ren waliandika mashairi ya nyimbo nyingi za kundi, ikiwa ni pamoja na "Fuck tha Police", wimbo ambao uliwasababishia migogoro na vyombo mbalimbali vya sheria. Chini ya shinikizo kutoka kwa Focus on the Family,[13] Milt Ahlerich, mkurugenzi msaidizi wa FBI alituma barua kwa Ruthless na kampuni yake ya usambazaji ya Priority Records, akiwashauri wasanii hawa kwamba "kutetea vurugu na mashambulizi ni makosa na sisi katika jumuiya ya watekelezaji sheria tunapinga hatua kama hiyo." Barua hii ipo katika Jumba la Umaarufu la Rock na Roll huko Cleveland, Ohio. [14]Polisi walikataa kutoa ulinzi kwenye matamasha ya kundi hili, na kuathiri mipango yao ya kufanya ziara. Hata hivyo, barua ya FBI ilisaidia kuvutia utangazwaji zaidi wa kundi.

Straight Outta Compton pia ilikuwa mojawapo ya albamu za kwanza kutolewa zikiwa na nembo ya Parental Advisory. Asili ya muziki wa N.W.A uliongeza mvuto wake kwa watu wengi. Mwezi mmoja baada ya kutolewa kwa albamu ya Straight Outta Compton, albamu binafsi ya kwanza ya Eazy-E, Eazy-Duz-It ilitolewa. Kwa sehemu kubwa albamu hiyo ilifanywa na Eazy (MC Ren alikuwa rapa pekee aliyeshirikishwa) lakini nyuma ya pazia ilikuwa juhudi za kundi.

Muziki ulitayarishwa na Dr. Dre na DJ Yella; nyimbo ziliandikwa kwa sehemu kubwa na MC Ren, pamoja na michango kutoka kwa Ice Cube na The D.O.C. Kwa studio za Ruthless, albamu hii ilikuwa mafanikio mengine ya kufikia mauzo ya platinamu.[15]

Wanachama

Kalenda ya matukio

Wasifu

Wawakilishi wa New Line Cinema walitangaza kupitia Entertainment Weekly "Hollywood Insider Blog" kwamba hadithi ya N.W.A ilikuwa ikiandaliwa ili kuwa filamu. Filamu ilifanyiwa utafiti na kuandikwa na mtengenezaji wa filamu S. Leigh Savidge na mfanyakazi mkongwe wa redio Alan Wenkus, ambaye alifanya kazi kwa karibu na mjane wa Eazy-E, Tomica Woods-Wright.[16] Ice Cube na Dr. Dre walishiriki kama watayarishaji wa filamu hiyo. Mnamo Septemba 2011, John Singleton alichaguliwa kama muongozaji. Hapo awali, Ice Cube na Singleton walishirikiana kwenye Boyz n the Hood, filamu ambayo iliwania Tuzo za Akademi, na Ice Cube pia aliigiza kama "Fudge" kwenye filamu ya Higher Learning, filamu hii ilitengenezwa na Singleton.[17]

Kutafuta waigizaji kulianza majira ya joto ya mwaka 2010. Kulikuwa na uvumi wa Lil Eazy-E kuigiza nafasi ya baba yake marehemu Eazy-E, na mtoto wa Ice Cube O'Shea Jackson Jr kuigiza nafasi ya baba yake pia.

Mnamo Agosti 2012, F. Gary Gray alichaguliwa kama muongozaji badala ya Singleton.[18] Filamu hiyo iliyopewa jina la Straight Outta Compton, ilikuwa imechukuliwa na Universal Pictures ambao walimwajiri Jonathan Herman [19]mnamo Desemba 2013 ili kuiandaa upya na ilimleta Will Packer kama mtayarishaji mkuu.[20] [21]Mnamo Februari 21, 2014, muongozaji F. Gary Gray kupitia ukurasa wake wa Twitter alitangaza mwito wa wazi wa nafasi za kuigiza filamu hiyo. [22] Rapa YG alijaribiwa kuigiza MC Ren katika filamu.[23]

Mnamo Juni 18, 2014, Universal ilitangaza kuwa filamu ya N.W.A Straight Outta Compton itatolewa Agosti 14, 2015. Mtoto wa Ice Cube, O'Shea Jackson Jr., aliigiza nafasi ya baba yake kwenye filamu, huku Jason Mitchell akiigiza Eazy-E, Corey Hawkins akiigiza Dr. Dre, Aldis Hodge akiigiza MC Ren, na Neil Brown Jr. akiigiza DJ Yella.[24][25][26] Filamu hii ilipokea maoni chanya na ilingiza zaidi ya dola milioni 200.

Urithi

"Chata la "Fuck the police" huko Cairo, 2011

Ingawa kundi hili lilisambaratika mwaka wa 1991, linasalia kuwa mojawapo ya makundi yenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye hip-hop, limeacha historia ya kudumu kwenye muziki wa hip hop.

Katika wimbo wa Dr. Dre wa mwaka 1999 "Forgot About Dre", Eminem anatoa heshima kwa kundi hili, akirap "So what do you say to somebody you hate / Or anyone tryna bring trouble your way? / Wanna resolve things in a bloodier way? / Just study a tape of N.W.A", akirejelea mapokezi mabaya ya kazi za N.W.A kwenye redio ambazo ziliona nyimbo za kundi hili kuwa za vurugu.[27] Tukio katika video ya wimbo wa The Game aliomshirikisha 50 Cent mwaka 2005 "Hate It or Love It" linaonyesha Tequan Richmond na Zachary Williams (wakiigiza kama The Game na 50 Cent) wakikamatwa na polisi baada ya kuchora chata la "N.W.A" ukutani. The game pia ana tattoo ya "N.W.A" upande wa kulia wa kifua chake.

Diskografia

Chata la nembo ya N.W.A

Studio albamu

EP(Extended plays)

Albamu za mkusanyiko

Ziara

Marejeo

  1. Potter, Russel A. (1995). Spectacular Vernaculars: Hip-Hop and the Politics of Postmodernism. New York City: State University of New York Press. uk. 50. ISBN 0-7914-2626-2.
  2. "Ice Cube produces N.W.A biopic". Filmstarts.de. Iliwekwa mnamo 2010-10-14.
  3. Erlewine, Stephen Thomas. [N.W.A katika Allmusic "N.W.A. Biography"]. allmusic. Iliwekwa mnamo 2007-08-17. {{cite web}}: Check |url= value (help)
  4. Former N.W.A manager Otto Kaiserauer talks gangsta rap
  5. White, Miles (2011). From Jim Crow to Jay-Z: Race, Rap and the Performance of Masculinity. Urbana, Illinois: University of Illinois Press. ku. 64, 74. ISBN 978-0-252-03662-0.
  6. Adrienne Green (2015-08-14). "'Straight Outta Compton' Points to What's Missing in Modern Hip-Hop". The Atlantic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-31.
  7. Erlewine, Stephen Thomas. [N.W.A katika Allmusic "N.W.A. Biography"]. allmusic. Iliwekwa mnamo 2007-08-17. {{cite web}}: Check |url= value (help)
  8. "N.W.A Songs, Albums, Reviews, Bio & More". AllMusic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-31.
  9. "Rolling Stone : The Immortals". web.archive.org. 2006-10-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-17. Iliwekwa mnamo 2022-05-31.
  10. "Aftermath Music dot com | Dr. Dre Eminem 50 Cent Busta Rhymes Stat Quo Eve Bishop Lamont G.A.G.E." www.tenerifehotel.net. Iliwekwa mnamo 2022-05-31.
  11. N.W.A N.W.A and the Posse Album Reviews, Songs & More | AllMusic (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2022-05-31
  12. Duff, S.L. N.W.A. YA BOY Biography. Yahoo! Music. Retrieved August 17, 2007.
  13. Nuzum, Eric (2001). Parental Advisory: Music Censorship in America. New York City: HarperCollins. uk. 111. ISBN 0-688-16772-1.
  14. Facebook, Twitter, Show more sharing options, Facebook, Twitter, LinkedIn (2008-08-16). "Mark of tha gangsta". Los Angeles Times (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-06-01. {{cite web}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  15. "Biography #5 | Amazing Pictures and Wallpapers | World Amazing Pictures and HD Wallpapers". web.archive.org. 2016-01-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-27. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.
  16. "'Compton' writer is straight outta Seattle". The Seattle Times (kwa American English). 2015-08-18. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.
  17. HipHopDX- https://hiphopdx.com (2014-02-22). "Ice Cube Wants His Son O'Shea To Play Him In N.W.A Biopic". HipHopDX. Iliwekwa mnamo 2022-06-01. {{cite web}}: External link in |author= (help)
  18. Homie, Big. (August 13, 2012) N.W.A Movie Begins Filming Archived Agosti 29, 2013, at the Wayback Machine. Rap Radar. Retrieved on 2014-04-11.
  19. "Jonathan Herman". IMDb. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.
  20. Max Weinstein, Max Weinstein (2013-12-19). "N.W.A. Biopic 'Straight Outta Compton' Brings On Writer". VIBE.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-06-01.
  21. Archive-Sophie-Schillaci. "N.W.A Casting Call: Who Should Play Ice Cube, Dr. Dre In 'Straight Outta Compton'?". MTV News (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-05-29. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.
  22. Director F. Gary Gray Announces Open Casting Call For N.W.A. Biopic (Details) | Shadow and Act "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-19. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.. Blogs.indiewire.com. Retrieved on April 11, 2014.
  23. The Breakfast Club Interviews YG & DJ Mustard "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-07. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.. Rap Radar (March 21, 2014). Retrieved on 2014-04-11.
  24. Lee, Ashley (Juni 18, 2014). "[PHOTO] N.W.A. Biopic 'Straight Outta Compton' First Look". Hollywood Reporter. Iliwekwa mnamo Julai 26, 2015.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  25. "NWA Biopic 'Straight Outta Compton' Finds Its MC Ren and DJ Yella". Movieweb.com. Julai 29, 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-12. Iliwekwa mnamo Julai 26, 2015. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. Perlman, Jake (Julai 29, 2014). "Casting Net: N.W.A biopic 'Straight Outta Compton' completes casting". Entertainment Weekly. Iliwekwa mnamo Machi 3, 2020.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  27. Dr. Dre (Ft. Eminem) – Forgot About Dre, iliwekwa mnamo 2022-06-01
  28. Woldu, Gail (2008). The Words and Music of Ice Cube. Westport, Connecticut: Greenwood Publishing Group. ku. 21–22. ISBN 0-275-99043-5.
  29. DeVito, Lee. "The real story behind N.W.A.'s 'Straight Outta Compton' Detroit riot". Detroit Metro Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-27. Iliwekwa mnamo Juni 25, 2021. {{cite news}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  30. "Power 97". Power97.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-04-01. Iliwekwa mnamo Juni 25, 2021. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  31. Bells, Rock The. "Hip-Hop Label 101: Priority Records". Rock The Bells. Iliwekwa mnamo Juni 25, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Vingo vya Nje

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!