Mjukuu ni mtoto wa mwanao, bila kujali jinsia yako wala yake. Yeye anakuita babu au bibi.[1]
Mtoto wake tena anaitwa kitukuu, mtukuu au kusukuu.[1]
Katika Kiswahili ni maarufu mithali inayosema, "Majuto ni mjukuu", kwa maana mara nyingi jambo la hatari ulifanyapo kwa wakati husika, waweza kujuta baadaye.[2]