Manga

Herufi ya lugha ya Kijapani kutoka kitabu Seasonal Passersby (Shiki no Yukikai), 1798, kilichotungwa na Santō Kyōden na Kitao Shigemasa.

Manga (ja: 漫画 kanji: まんが katakana: マンガ English: /ˈmɑːŋɡə/) ni hadithi zinazotungwa kwa kutumia michoro (wakati mwingine pia hujulikana kama komikku katika lugha ya Kijapani). Hufuata jinsi ya kuchora ulioendelezwa Ujapani mwishoni mwa karne ya 20. Katika namna zake za kisasa, manga zilianza muda mfupi baada ya Vita vikuu vya pili [1], lakini aina hii ya sanaa ina historia ndefu katika miaka awali ya sanaa ya Ujapani.

Katika Ujapani, watu wa umri wote husoma manga. Manga ni aina ya sanaa inayojumuisha mapana ya mada kama vile: "action-adventure", mapenzi (kWa Kiingereza romance), michezo (sports and games), drama za kihistoria (historical dramas), vichekesho (comedy), bunilizi za kisayansi (science fiction), fumbo (mystery), hadithi ya kutisha (horror), ngono (sexuality), na biashara (business and commerce), miongoni mwa nyingine. [2]

Tangu miaka ya 1950, manga imekua na kujiendeleza; hadi sasa inawakilisha sehemu kubwa ya sekta ya kuchapisha humo Ujapani, ni sekta iliyowakilisha yen bilioni 406 katika soko nchini Japan mnamo mwaka 2007 (wastani wa dola bilioni 3.6). Manga imekuwa maarufu duniani kote pia. [3] Mwaka wa 2008, soko la manga katika nchi za Marekani na Kanada ilikuwa $ milioni 175.

Manga kwa kawaida huchapishwa bila rangi, yaani huwa nyeusi-na-nyeupe, ingawa kuna baadhi ya manga zinazochapishwa kutumia rangi zote. Katika Ujapani, manga kawaida huchapishwa katika vitabu vyenye kurasa nyingi, huenda vitabu hivi huhusisha hadithi tofauti, na kila hadithi huendelezwa katika suala la kufuata. Mfululizo ukiwa na mafanikio, sura zilizokusanywa zinaweza kuchapishwa tena katika vitabu viitwayo tankōbon. [4] Msanii wa manga (mangaka kwa Kijapani) kawaida hufanya kazi na wasaidizi wachache katika studio ndogo na pamoja na mhariri kutoka kampuni ya kuchapisha. [1] Manga ikiwa maarufu inaweza kubadilishwa kuwa kipindi kinachoweza kutazamwa katika runinga baada au hata wakati ambako inachapishwa, [5] Wakati mwingine manga zinazohusisha filamu zilizopo awali hutunzwa (k.m. Star Wars).

Neno "Manga" hutumika nje ya Ujapani kumaanisha vitabu vya michoro viliyochapishwa nchini Ujapani. [6] Hata hivyo, vitabu vya michoro vilivyoshawishiwa kutoka manga vipo katika maeneo mengine ya dunia, hasa katika Taiwan (manhua), Korea ya Kusini (manhwa) [7] na Jamhuri ya Watu wa China, hasa Hong Kong (manhua). [8] Katika Ufaransa, la Nouvelle manga ina maendeleo kama aina ya bande dessinée (yaani drawn strip) inayotolewa katika mitindo iliyoshawishiwa na manga kutoka Ujapani. Katika Marekani, watu hurejelea vitabu vinavyofanana na manga kama Amerimanga, manga ya dunia, au manga yenye asili ya lugha ya Kiingereza ("original english language manga" - OEL manga).

Asili ya jina

Neno la Kijapani manga, likitafsiriwa vizuri lina maana ya "whimsical pictures". Matumizi ya kawaida ya neno ya Kijapani Manga yalianza mwishoni mwa karne ya 18 wakati ambako kazi kama vile Shiji no yukikai iliyotunzwa na Santo Kyōden ilichapishwa mwaka 1798, na katika karne ya 19 wakati ambako kazi kama Manga Hyakujo (1814) iliyotunzwa na Aikawa Minwa ilichapishwa pamoja na manga iliyosifiwa jinale Hokusai Manga ikiwa na michoro kutoka msanii maarufu wa sanaa iitwayo ukiyo-e jinale Hokusai. [9] Rakuten Kitazawa (1876-1955) kwanza alitumia neno "manga" katika hali ya kisasa. [10]

Historia na sifa

Wanahistoria na waandishi wanaoelezea historia ya manga hutaja michakato mbili pana na nyongeza iliyochangia manga kisasa. Maoni yao yanatofautiana katika umuhimu wanayoipa nafasi ya matukio ya kiutamaduni na kihistoria zifuatazo Vita Kuu II dhidi ya jukumu la sanaa na utamaduni Kijapani zilizopo kabla ya Vita Kuu II Meiji na kabla ya Meiji.

Oni moja inasisitiza matukio yanayotokea wakati wa na baada ya ukaazi wa Marekani katika Ujapani (1945-1952), na inasisitiza kuwa manga ilishawishiwa sana na utamaduni za Marekani, ikiwemo vitabu vya michoro kutoka Marekani (vilivyoletwa kwa Ujapani na wanajeshi) na picha na mandhari kutoka televisheni, filamu, na katuni (hasa Disney) kutoka Marekani [11] Aidha waandishi wengine kama Frederik Yale Schodt, Kinko Ito, na Adam Yale Kern husisitiza mwendelezo wa utamaduni na mila estetika Kijapani kama kati ya historia ya manga. [12]

Manga ya kisasa ina asili katika Ukaazi (1945-1952) na miaka baada ya Ukaazi wa Marekani(1952-miaka ya mapema ya 1960), wakati ambako Ujapani uliokuwa unautegemea sana utawala wa Jeshi na kusisitiza uaminifu kwa nchi hapo awali ulikuwa unajijenga upya katika miundombinu ya kisiasa na kiuchumi. Mlipuko wa ubunifu wa kisanaa ulitokea katika kipindi hiki, [13] ulishirikisha wasanii wa manga kama vile Osamu Tezuka (Astro Boy) na Machiko Hasegawa (Sazae-san).

Hadithi ya aina ya kami-shibai kutoka Sazae-san iliyotungwa na Machiko Hasegawa. Sazae anaonyeshwa akiwa amefunga nywele yake.

Astro Boy ilipata (na inabakia kuwa na) umaarufu mkubwa katika Ujapani na mahali pengine, [14] na marekebisho katika vibonzo viitwavyo anime ya Sazae-san inaendelea kuonyeshwa runingani mara huwa na watazamaji zaidi kuliko anime nyingine yoyote kwa televisheni Kijapani. Tezuka na Hasegawa wote walileta uvumbuzi katika ubunifu wa manga. Tezuka alitumia mbinu iitwalo "Cinematographic", ambako kila picha ilionyesha maelezo ya hatua kutoka mwendo wa polepole inayopakana na mwendo wa kasi na vilevile msongo kutoka picha inayonyesha umbali na karibu. Aina hii ya ubinifu ulifuatwa na wasanii wengine baadaye. [15] Hasegawa ambaye alizingatia maisha ya kila siku na uzoefu wa wanawake pia alikuja baadaye kushawishi aina ya manga iitwalo shōjo manga. [16] Kati ya 1950 na 1969, mwongezeko mkubwa wa wasomaji wa manga ulijitokeza katika Ujapani baada ya uungano wa masoko kuu mawili ya wasomaji manga, yaani manga ya wasomaji kiume au shōnen manga na manga iliyokuwa na lengo ya wasomaji wasichana au shōjo manga.

Katika mwaka wa 1969 kikundi cha wasanii wanawake wa manga (kiitwacho Year 24 na kilichojulikana kama Magnificent 24s awali), walichapishashōjo manga yao ya kwanza ("mwaka 24" linatokana na jina Kijapani ya 1949, katika wasanii wengi hawa walizaliwa). [17] Kundi huu ulihusisha Hagio Moto, Riyoko Ikeda, Yumiko Oshima, Keiko Takemiya na Ryoko Yamagishi, waliokuwa wanawake wa kwanza kuingia dunia ya manga. [4] Baada ya hapo, hasa wasanii wanawake ndio waliochora shōjo manga kwa usomaji wa wasichana na wanawake vijana. [18] Katika miongo zifuatazo (1975-hadi leo),shōjo manga iliendelea kujiendeleza katika ubunifu na pia aina tofauti ya shojo manga zilijitokeza. Aina hizi ni kama vile hadithi vya mapenzi(romance), vya wanawake shujaa(suerheroines), na manga iiyolengwa kwa wanawake ((katika Kijapani, redisu, redikomi na josei).

Romance shōjo manga kisasa huhusisha pendo kama mada kuu. Katika shojo manga inayohusu wanawake mashujaa, manga ya Naoko Takeuchi iitwalo Pretty Soldier Sailor Moon ilijitokeza ikawa maarufu kimataifa katika anime na manga. [19] Makundi (au Sentai) ya wasichana wanaofanya kazi pamoja pia yamekuwa maarufu ndani ya hii aina ya manga. [20]

Manga kwa wasomaji wanaume ina mgawanyiko kulingana na umri wa wasomaji inayolengewa: wavulana hadi umri wa miaka 18 (shōnen manga) na wanaume vijana 18 - hadi umri wa miaka 30-(seinen manga); [21] pia manga hugawanyika kwa maudhui, kwa mfano manga yanayohusu "action-adventure" mara nyingi huwashirikisha wanaume mashujaa, ucheshi, mandhari ya heshima, na wakati mwingine kujamiiana. [22] Kuna jinsi mbili ya kuandika neno seinen katika Kijapani- moja ambayo inayorejelea maana 青年 ya "vijana, kijana" na 成年 nyingine inayorejelea maana ya "watu wazima" - ya pili ikitumiwa kueleza manga zinazohusisha kujamiiana zilizolengwa kwa wanaume wazima wanaoitwa seijin. Shōnen, seinen, naseijin kwa kawaida yanashirikisha mada nyingi zinazofanana.

Wavulana na wanaume vijana walikuwa baadhi ya wasomaji wa kwanza wa manga baada ya Vita Kuu II. Kuanzia miaka ya 1950, shōnen manga ililenga mada wasanii walidhani zingeridhisha wavulana kawaida kama vile hadithi kuhusu mashine (robots) na mashujaa[23] Mandhari maarufu ni sayansi, teknolojia na michezo. Manga yaliyohusisha wahusika shujaa wasiojihusisha na shujaa wengie kama vile Superman, Batman, na Spider-Man hazikuwa maarufu hasa. [24]

Jukumu la wasichana na wanawake katika manga zinazolengwa kwa wasomaji wanaume imebadilika sana kuhusisha wasicha warembo(bishōjo) [25] kama vile Belldandy kutoka manga iitwayo Oh My goddess!, hadithi ambapo wanawake na wasichana hawa warembo hujihusisha na mwanaume shujaa, kama katika Negima na Hanaukyo Maid Team, au makundi ya wanawake shujaa wanaobeba silaha (sento bishōjo) [26]

Baada ya udhibiti katika Ujapani kupunguzwa katika miaka awali ya muongo wa 1990, aina mbalimbali za manga zilizohusisha mandhari ya ngono zilianza kuchapishwa, manga hizi zililengwa kwa wasomaji wanume, na kutafsiriwa katika Kiingereza. [27] Manga hizi zilihusu wahusika waliochorwa wakiwa katika hali ya kuwa na mavazi kidogo sana au uchi kabisa na wakiwa wanahusika katika ngono. Huenda mandhari kuhusu mazoezi mwiko ya ngono kama vile ubakaji, ngono baina ya watu wa familia moja na ngono baina ya binadamu na wanyama na kadhalika.

Mtindo wa kuchora jinale Gekiga ni mtindo ambapo michoro hufanana sana na viumbe ambvyo vinachorwa. Manga zilizochorwa kufuata mtindo huu kwa kawaida hulenga maada kuhusu maisha ya kila siku [28] Gekiga kama vile Chronicles of a Ninja's Military Accomplishments (Ninja Bugeichō) iliyolengwa na Sampei Shirato katika miaka ya 1959 hadi 1962, zilijitokeza mwishoni mwa miaka ya 1950 na 1960 kutoka wanafunzi na waliohusika katika uanaharakati wa kisiasa wa mrengo wa kushoto [29] na kiasi kidogo kutokana na kutoridhika kwa manga zilizopo na wasanii wa manga vijana kama Yoshihiro Tatsumi [30]

Machapisho

Katika mwaka wa 2007 manga ilizalisha mapato ya dola mia nne na sita bilioni nchini Ujapani. Hivi karibuni, sekta ya manga imeenea kote duniani huku makampuni yakinunua leseni ya manga kutoka wachapishaji nchini Ujapani na kuzichapisha na kusambaza manga hizo katika lugha nyingine.

Baada ya mfululizo wa manga moa kuchapishwa kwa muda, wachapishaji mara nyingi hukusanya hadithi zote za manga hiyo pamoja katika vitabu, viitwavyo tankōbon. Vitabu hivi vinafanana kiumbo na riwaya. Tankobon hutumia karatasi bora zaidi, na ni muhimu kwa wale ambao wanataka kufuata manga inayochapishwa magazetini ikiwa hawakusoma machapisho ya awali au kama wao hupata gharama ya manga inayochapishwa katika magazeti kila wiki au mwezi kuwa kizuizi. Hivi karibuni, tankobon ziitwazo "Deluxe" zimechapishwa na hulengwa wa wasomaji wazima. Manga kutoka miaka yaliyopita pia zimechapishwa kutumia karatasi ya kiwango ya chini na ambayo huuzwa kwa dola $1 ili kushindana na sekta ya uuzaji wa vitabu vilivyotumika.

Kimsingi manga hutenganishwa kutegemea umri na jinsia ya wasomaji. [31] Hasa, vitabu na majarida yaliolengwa kwa wavulana (shōnen) na wasichana (shōjo) huwekwa kwenye rafu tofauti katika maduka ya vitabu vingi. Wasomaji huenda husoma manga ambazo zinalengwa kwa wasomaji wa umri au jinsia nyingie kwa ajili hii mwitikio wa wanunuzi wa manga haudhibitishwi na umri au jinsia ya wasomaj. Kwa mfano, wasomaji wa kiume wakisoma shojo manga.

Ujapani pia ina mikahawa iitwayo manga café, au manga kissa (kifupisho cha kissaten). Katika manga kissa, watu hunywa kahawa na kusoma manga, na wakati mwingine hukaa huko usiku kucha.

Kumekuwa na ongezeko katika kiasi cha webmanga au manga yanayochapishwa ili kusomwa katika mtandao. Huchorwa na mashabiki wa ngazi zote wa uzoefu. Inaweza kuamuriwa katika fomu ya riwaya.

Magazeti

Eshinbun Nipponchi; Inayojulikana kama gazeti la manga la kwanza

Magazeti ya manga kawaida huwa na mfululizo ya hadithi nyingi ambazo huchukua kurasa 20-40 zilizotengwa kwa kila hadithi kwa chapisho hilo. Magazeti mengine kama vile moja liitwalo Newtype huchapisha sura moja moja katika machapisho yao yanayosambazwa kila mwezi. Magazeti mengine kama Nakayoshi yanachapisha hadithi nyingi zilizoandikwa na wasanii mbalimbali, haya magazeti (au "anthology magazines" kama yanajulikana), kwa kawaida huchapishwa kwa kwa karatasi ya kiwango ya chini na yanaweza kuwa na kurasa 200 hadi hata 850. Magazeti haya pia yana hadithi ambazo hukamilika katika chapisho moja (one-shot) na aina mbalimbali ya hadithi ya michoro fupi mno ziitwazo yonkoma . Manga huweza kuchapishwa kwa miaka mingi kama ina mafanikio. Wasanii wa manga huanza kwa kutenga manga michache ya aina ya "one-shot" ili kupata kutambuliwa katika sekta ya manga. Kama hadithi haya mifupi yana mafanikio na hupokea hakiki mema, yanaendelezwa katika magazeti.

Historia

Kanagaki Robun na Kawanabe Kyosai waliumba gazeti la manga la kwanza katika mwaka wa 1874 jinale Eshinbun Nipponchi. Mwingereza mmoja aitwaye Charles Wargman alianzisha Japan Punch, ambalo lilishawishi gazeti hilo. Eshinbun Nipponchi ulitumia mtindo wa kuchora ambao haukupendeza na haukuwa maarufu kwa watu wengi. Eshinbun Nipponchi ulikamilishwa baada ya masuala matatu tu. Gazeti liitwaloKisho Shimbun ulitokana na Eshinbun Nipponchi, mnamo mwaka wa 1875 ilifuatiliwa na Marumaru Chinbun katika mwaka wa 1877, na kisha Garakuta Chinpo katika mwaka wa 1879. [32] Shōnen sekai lilikuwa gazeti la kwanza lililohusisha manga iliyolengwa kwa wasomaji wanaume na liliumbwa mwaka wa 1895 na Iwaya Sazanami, aliyekuwa mwandishi maarufu ya fasihi ya watoto Kijapani. Shōnen sekai ilizingatia mno vita baina ya Uchina na Ujapani kutoka mwaka wa 1894 hadi 1895 [33]

Mwaka wa 1905 uchapishaji wa magazeti ya manga ilienea mno kufuatilia Vita baina ya Urusi na Ujapani, [34] Tokyo Pakku liliundwa na lkawa maarufu sana. [35] Baada ya Tokyo Pakku k katika mwaka wa 1905, toleo la Shōnen sekai lililolengwa kwa wanawake liitwalo [[Shōjo sekai/1} lilichapishwa na kufikiriwa kama gazeti la kwanza la shojo manga. |Shōjo sekai/1} lilichapishwa na kufikiriwa kama gazeti la kwanza la shojo manga. [36]]] Shōnen Pakku liliundwa na hadi sasa hufikiriwa kuwa gazeti la kwanza lililolengwa kwa watoto (kodomo katika kijapanai). Aina ya manga iliyolengwa kwa kodomo ilikuwa katika hatua mapema ya maendeleo katika kipindi ya Meiji. Mwaka wa 1924, Kodomo Pakku ilizinduliwa kama gazeti la kodomo nyingine baada ya Shōnen Pakku. [35] Katika kipindi hiki cha uchapishaji wa magazeti mengi ya manga, gazeti liitwalo Poten lililochapishwa katika mwaka wa 1908. Kurasa zote katika gazeti hili yalitiwa rangi kufuatilia mtindo wa magazeti ya Tokyo Pakku na Osaka Pakku. Haijulikani kama kuna masuala mengine yoyote zaidi kuliko ya kwanza. [34] Kodomo Pakku ilizinduliwa mwezi wa Mei mwaka wa 1924 na Tokyosha. Ilihusisha michoro ya kiwango cha juu kutoka wasanii wengi katika jamii la usaani wa Manga kama Takei Takeo, Takehisa Yumeji na Aso Yutaka. Majadiliano ya wahusika kwenye baadhi ya manga haya yalionyeshwa kwa njia ya viputo vya maneno na jinsi hii ya kuwakilisha hadithi ilitofautiana na Manga yaliyochorwa awali ambazo hazikutumia viputo na hasa zilikuwa "kimya".

Manga no Kuni, gazeti lililoanzia mwezi wa Mei katika mwaka wa 1935 hadi mwezi wa Januari mwaka wa 1941 lilihusisha habari kuhusu jinsi ya kuwa msaani wa Manga yaani mangaka na pia habari kuhusu viwanda vingine vya vibonzo duniani kote. Manga no Kuni lilipatia jina lake kwa gazeti jingine lililojulikana kama Sashie Manga Kenkyū mwezi Agosti mwaka wa 1940. [37]

Dōjinshi

Dōjinshi ni aina ya manga zilizotayarishwa na wachapishaji wasiostadi na ambazo hasa huanguka nje ya mkondo mkuu wa biashara ya uchapishaji wa manga. Comiket, ni mkutano mkuu ya mashabiki wa manga (wasomaji na wasanii)ambao huvutia idadi ya watu inayopita 510,000 kila mwaka. Hasa mkutano huh hujishugulisha na dojinshi . Mara nyingi hadithi zilizohusishwa katika dojinshi yana asili huru lakini kuna baadhi ya hadithi ambazo zimeshawishiwa na manga na anime zilizoimarishwa awali. Baadhi ya dōjinshi huendeleza hadithi fulani au huhusisha wahusika wa hadithi fulani katika tunzo nyingine na huwa kama fan fiction yaani hadithi iliyotunzwa na mashabiki. Mwaka wa 2007, dōjinshi ziliuzwa kwa bilioni za yen 27.73(milioni za dola 245).

Masoko ya kimataifa

Kutoka mwaka wa 2007 ushawishi wa manga katika sekta ya usanii wa komiki( kutoka Kiing. comic)duniani ulikuwa umezidi katika miongo miwili awali. [38] Ushawishi inahusu jinsi manga zilivyoathiri masoko ya komiki nje ya Ujapani na pia jinsi zilivyoathiri estetika (kutoka Kiingereza aesthetic) ya wasanii kimataifa.

Mwelekeo wa kusoma Manga

Kijadi, mtiririko wa hadithi katika manga hutoka juu hadi chini na upande wa kulia hadi wa kushoto, kufuatia muundo wa jadi katika uandishi wa lugha ya Kijapani. Baadhi ya wachapishaji ya manga iliyotafsiriwa hubadilisha muundo ili mwelekeo wa kusoma ni wa kushoto kwenda kulia, ili kutochanganyisha wasomaji wageni. Mazoezi haya hujulikana kama "flipping". [39] Ukosoaji kuhusu ubadilishaji wa mwelekeo asili ya manga ni kama vile kuwa ubadilishaji huenda kinyume na matakwa ya mangaka kwa mfano: Ikiwa neno lilioandikwa kwa shati la mhusika lilikuwa "MEI", baada ya ubadilishaji huenda neno hilo hubadilika kuwa "IEM". Pia husababisha michanganyik kwa vitu , kama vile shati kuwa na vifungo kwa upande hazifai kuwa.

Marekani

Manga ilijiingiza polepole tu katika masoko ya Marekani, kwanza katika muungano na anime na kisha kujitegemea huru. [40] Baadhi ya mashabiki Marekani walikuwa na fahamu ya manga katika miaka ya 1970 na miaka ya 1980. Hata hivyo awali, anime ilipatikana zaidi kuliko manga katika mashabiki nchini Marekani, [41] wengi ambao walikuwa na umri wa 18 hadi 22. Kupata, kutafsiri na kuonyesha kanda za anime kulikuwa rahisi kuliko kutafsiri, kutoa nakala na kusambaza tankōbon vya manga. Manga ya kwanza kutafsiriwa katika Kiingereza na kuuzwa katika Marekani ni Barefoot Gen kutoka msanii jinale Keiji Nakazawa ni ambalo lilikuwa hadithi tawasifu kuhusu Mlipuko wa mabomu chembe( yaani Atomic) katika Hiroshima , iliyotolewa na wachapishaji Leonard Rifas na Educomics (1980-1982). Manga nyingine zilizotafsiriwa kati ya katikati ya miaka ya 1980 na 1990 ni kama vile, Golgo 13 (1986), Lone Wolf and Cub kutoka First Comics (1987). Kamui, Area 88, na Mai the Psychic Girl, yalichapishwa mwaka wa 1987 kutoka Viz Media-Eclipse Comics. [42] Manga nyingine zilizofuata ni Akira kutoka Marvel Comics - Epic Comics na Appleseed kutoka Vibe Comics mwaka wa 1988, na baadaye Iczer-1 kutoka Antarctic Press (1994) na baadaye F-111 Bandit iliyoandikwa na kuchorwa na Ippongi Bang iliyochapishawa na Antarctic Press (1995).

Katika miaka ya 1980 hadi katikati ya miaka ya 1990, anime kama Akira, Dragon Ball, Neon Genesis Evangelion, na Pokémon, zilikuwa na athiri kubwa zaidi katika uzoefu wa mashabiki na katika soko kuliko manga. [43] Masuala yalibadilika wakati mtafsiri na mjasiriamali Toren Smith alianzisha kampuni liitwalo Proteus Studio mwaka wa 1986. Smith na Studio Proteus walijifanya kama kikali na watafsiri wa manga nyingi, kama vile Appleseed kutoka Masamune Shirow na Oh My goddess! kutoka Kosuke Fujishima kwa niaba ya wachapishaji wa Dark Horse na Eros Comix, ili kuondoa haja ya wachapishaji hawa kutafuta mawasiliano yao binafsi katika Ujapani. [44]

Kijana akisoma manga jinalo Black Cat katika duka moja ya Barnes and Noble nchini Marekani.

Soko la manga nchini Marekani lilipata usaidizi katikati ya miaka ya 1990 ambamo manga na anime ya Masamune Shirow jinale Ghost in the Shell (iliyotafsiriwa na Frederik Yale Schodt na Toren Smith) ilipata umaarufu sana miongoni mwa mashabiki Marekani. Manga nyingine iliyopata mafanikio katikati ya miaka ya 1990 ilikuwa Sailor Moon. [45] Katika miaka ya 1995 hadi 1998, manga ya Sailor Moon iliuzwa katika nchi zaidi ya 23 kama vile Uchina, Urusi, Uitaliani na Amerika Kaskazini. [46] Mwaka wa 1997, jumba la uchapishaji jinale Mixx Entertainment ilianza kuchapisha, Sailor Moon, pamoja na manga kutoka jumba la uchapisaji nchini Ujapani CLAMP iitwayo [[Magic Knight Rayearth, Parasyte iliyotunzwa na Hitoshi Iwaaki na Ice Blade iliyotunzwa na Tsutomu Takahashi, katika gazeti la manga lililotolewa kila mwezi jinalo MixxZine.|Magic Knight Rayearth, Parasyte iliyotunzwa na Hitoshi Iwaaki na Ice Blade iliyotungwa na Tsutomu Takahashi, katika gazeti la manga lililotolewa kila mwezi jinalo MixxZine. ]] Miaka miwili baadaye, MixxZine lilipewa jina Tokyopop kabla ya kukamilishwa mwaka wa 2000.

Katika miaka iliyofuata, manga ilipata umaarufu, wachapishaji wapya waliingia soko. [47] As of 2008 Soko ya manga nchini Marekani na Kanada yalizoa mapato ya milioni ya dola 175 kwa mauzo ya mwaka. [48] Sambamba, mkondo mkuu wa habari nchini Marekani ilianza kujadili manga, katika makala katika magazeti kama The New York Times, Time magazine, The Wall Street Journal, na Wired magazine. [49]

Uropa

Manga kilifunguliwa katika soko la Ulaya katika miaka ya 1970 ambako Italia na Ufaransa yalionyesha anime katika runinga. [50] Sanaa ya Kifaransa imekopa kutoka Ujapani tangu karne ya 19 (Japonisme), [51] Manga umeonyesha umaarufu sana kwa upana wa wasomaji, karibu asilimia 30% ya mauzo ya komiki nchini Ufaransa ni ya manga tangu mwaka wa 2004. [52] Kulingana na Shirika la Biashara inyotendeka nje ya Ujapani, mauzo ya manga yalifika milioni za dola 212.6 ndani ya Ufaransa na Ujerumani pekee mwaka wa 2006. [50]

Wachapishaji Ulaya pia hutafiri manga katika lugha nyingine kama vile Kijerumani, Kiitaliano, Kiholanzi, na kadhalika. Wachapishaji wa manga waptikanako nchini Uingereza ni Titan pamoja na Gollancz Books. Wachapishaji wa manga kutoka Marekani pia wana nguvu katika masoko ya Uingereza, kwa mfano, Tanoshimi kutoka jumba la uchapishaji jinalo Random House.

Tuzo

Kuna Tuzo za aina tofauti katika sekta la usanii wa Manga zinazotolewa kwa wasanii stadi kila mwaka. Mifano ya tuzo hizi ni kama vile:

  • Akatsuka tuzo inayotoewa kwa manga inayochekesha kuliko zote nyingine.
  • Dengeki Grand Prix Comic inyotolewa kwa manga ya aina ya "one-shot".
  • Kodansha (tuzo inayotolewa kwa manga inayohusisha maada ya aina tofauti)
  • Seiun( Tuzo la manga inayohusu hadithi chuku za sayansi (Katika Kiing. "Science Fiction")
  • Shogakukan (inayotolewa kwa manga inayohusisha maada tofauti)
  • Tezuka (inayotolewa kwa manga bora inayochapishwa kwa mfululizo)
  • Tezuka Osamu "Cultural Prize"(inayotolewa kwa manga inayohusisha maada tofauti)

Kutokea mwaka wa 2007, Wizara ya Masuala ya Kigeni hutoa tuzo iitwayo "International Manga Award".

Tazama pia

Tanbihi

  1. 1.0 1.1 Kinsella 2000
  2. Gravett 2004, p. 8
  3. Wong 2006 Patten 2004
  4. 4.0 4.1 Gravett 2004, p. 8 Schodt 1986
  5. Kittelson 1998
  6. Merriam-Webster 2009
  7. Webb 2006
  8. Wong 2002
  9. Bouquillard & Marquet 2007
  10. Shimizu 1985, p. 53–54, 102–103
  11. Kinsella 2000 Schodt 1986
  12. Schodt 1986 Ito 2004 Kern 2006 Kern 2007
  13. Schodt 1986 Schodt 1996 Schodt 2007 Gravett 2004
  14. Kodansha 1999, pp. 692–715 Schodt 2007
  15. Schodt 1986
  16. Gravett 2004, p. 8 Lee 2000 Sanchez 1997–2003
  17. Gravett 2004, pp. 78–80 Lent 2001, pp. 9–10
  18. Schodt 1986 Toku 2006 Thorn 2001
  19. Allison 2000, pp. 259–278 Schodt 1996, p. 92
  20. Poitras 2001
  21. Thompson 2007, pp. xxiii–xxiv
  22. Brenner 2007, pp. 31–34
  23. Schodt 1986, pp. 68–87 Gravett 2004, p. 52–73
  24. Schodt 1986, pp. 68–87
  25. Perper & Cornog 2002, pp. 60–63
  26. Gardner 2003
  27. Perper & Cornog 2002
  28. Schodt 1986, p. 68–73 Gravett 2006
  29. Schodt 1986, p. 68–73 Gravett 2004, pp. 38–42 Isao 2001
  30. Isao 2001, pp. 147–149 Nunez 2006
  31. Schodt 1996
  32. Eshinbun Nipponchi
  33. Griffiths 2007
  34. 34.0 34.1 Poten
  35. 35.0 35.1 Shonen Pakku
  36. Lone 2007, p. 75
  37. Manga no Kuni
  38. Pink 2007 Wong 2007
  39. Farago 2007
  40. Patten 2004
  41. Napier 2000, pp. 239–256 Clements & McCarthy 2006, pp. 475–476
  42. Patten 2004, pp. 37, 259–260 Thompson 2007, p. xv
  43. Leonard 2004 Patten 2004, pp. 52–73 Farago 2007
  44. Schodt 1996, pp. 318–321 Dark Horse Comics 2004
  45. Patten 2004, pp. 50, 110, 124, 128, 135 Arnold 2000
  46. Schodt 1996, p. 95
  47. Schodt 1996, pp. 308–319
  48. Reid 2009
  49. Glazer 2005 Masters 2006 Bosker 2007 Pink 2007
  50. 50.0 50.1 Fishbein 2007
  51. Berger 1992
  52. Mahousu 2005 ANN 2004 Riciputi 2007

Marejeo

Marejeleo zaidi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!