Lugha za Kiturki ni kundi la lugha zaidi ya 30 zinazozungumzwa kutoka Ulaya ya Mashariki hadi Asia ya Kati na watu milioni 210. Zinahesabiwa kuwa sehemu za lugha za Kialtai pamoja na Kichina, Kimongolia, Kijapani na Kikorea. Wasemaji wa lugha za Kiturki husikizana kwa kiasi kikubwa. Lugha ya Kiturki inayojulikana zaidi kimataifa pia yenye wasemaji wengi ni Kituruki cha Uturuki.
Asili ya wasemaji wa lugha za Kiturki inadhaniwa kuwa sehemu za Mongolia. Kati ya karne za 6 hadi 10 walisambaa hadi Asia ya Magharibi na baada ya kutwaa Milki ya Bizanti waliingia pia katika Ulaya ya kusini-mashariki.
Lugha za Kiturki zenye wasemaji wengi
Lugha tatu kubwa za kundi hili ni
Kituruki wasemaji milioni 60 katika Uturuki na vikundi vidogo katika nchi za Balkani; kutokana na uhamiaji pia katika nchi za Ulaya ya Kati na ya Magharibi (Ujerumani, Uholanzi)
Kitshuwashi wasemaji milioni 1.8 katika Urusi (sehemu ya kiulaya)
Kibashkiri wasemaji milioni 2.2 katika Bashkiria jamhuri ya shirikisho la Urusi
Kitartari wasemaji milioni 1.6 kati ya Urusi ya kati hadi Sibiria
Kikashgai wasemaji milioni 1,5 Mio Sprecher katika majimbo ya Uajemi ya Fars na Khuzistan
Mifano ya maneno ya lugha za Kiturki
Mifano ifuatayo inaonyesha jinsi gani lugha za Kiturki zinavyofanana:
Kiswahili
Kiturki cha Kale
Kituruki
Kiturkmeni
Kitatari
Kikazakhstan
Kiuzbeki
Kiuiguri
Mama
ana
anne/ana
ene
ana
ana
ona
ana
pua
burun
burun
burun
boryn
murın
burun
burun
mkono
qol
kol
qol
kul
qol
qo'l
kol
barabara
jol
yol
ýol
jul
zhol
yo'l
yol
mnene
semiz
semiz
semiz
simyz
semiz
semiz
semiz
ardhi
topraq
toprak
topraq
tufrak
topıraq
tuproq
tupraq
damu
qan
kan
gan
kan
qan
qon
qan
majivu
kül
kül
kül
köl
kül
kul
kül
maji
suv
su
suw
syw
suw
suv
su
nyeupe
aq
ak
ak
ak
aq
oq
aq
nyeusi
qara
kara
gara
kara
qara
qora
qara
nyekundu
qyzyl
kızıl
qyzyl
kyzyl
qızıl
qizil
qizil
anga
kök
gök
gök
kük
kök
ko'k
kök
Makala hii kuhusu "Lugha za Kiturki" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.