Kituo cha transfoma (kwa ing.electrical substation) ni kituo tanzu katika mfumo wa kuzalisha na kusambaza umeme ambapo volteji inabadilishwa kutoka juu hadi chini au kinyume chake kwa kutumia transfoma[1]. Nishati ya umeme inaweza kutiririka kupitia vituo vya transfoma kadhaa kati ya kituo cha kuzalisha kwa upande mmoja na watumiaji kwa upande mwingine. Humo volteji ya umeme unaweza kubadilishwa mara kadhaa.
Ilhali umeme hufika kwa mtumiaji kama mkondo geu kwa volteji ya volti 230, unapitishwa kwenye nyaya kwa umbali mkubwa kwa umbo la mkondo mnyofu wenye volti elfu kadhaa. Kwa hiyo vituo vya transfoma vinahitajika kubadilisha mkondo wa umeme kutoka volteji ya juu kwa umbali mkubwa hadi volteji ya kati kwa umbali mdogo hadi volteji ya V 230 kwa matumizi ya nyumbani.