Kisiwa cha Mombasa kinapatikana kwenye bahari ya Hindi karibu sana na pwani ya nchi ya Kenya na kinaunganishwa na bara kupitia "Makupa Causeway" upande wa Magharibi, daraja la Nyali upande wa Kaskazini na kivuko cha Likoni upande wa Kusini.
Mji wa kale wa Mombasa upo upande wa Mashariki mwa ufuo wa kisiwa hicho. Kilindini na Port Reitz ndiyo bandari za kisasa zenye vina virefu na zinatenganisha kisiwa na bara la Kenya kwa upande wa kusini.
Bandari ya kale inayojulikana kama Tudor na ilitumika kulinda Fort Jesus na Tudor Creek zinatenganisha kisiwa na bara upande wa Kaskazini. Maeneo ya kisasa ya makazi na maeneo ya viwanda yanapatikana kwenye sehemu nyingine za kisiwa.
Bandari ya Tudor na Tudor Creek zilipata majina yake kutoka kwa nahodhaOwen Tudor wa Royal Navy ambaye alikuwa wa kwanza kutafiti eneo hilo.
Ukurasa huu na makala haya ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuiboresha zaidi.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Mombasa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!