Kigong'ota

Kigong'ota
Kigong'ota mkia-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Picidae (Ndege walio na mnasaba na vigong'ota)
Nusufamilia: Picinae (Ndege walio na mnasaba sana na vigong'ota)
Ngazi za chini

Jenasi 27; spishi 32 katika Afrika:

Vigong'ota, gongonola, gogota, vigotagota au ving'ota ni ndege wa nusufamilia Picinae katika familia Picidae. Ni bora kutengea spishi za nusufamilia Picumninae jina “kigogota”. Inawakilishwa katika Afrika na kigogota wa Afrika. Vigong'ota vinatokea misituni na maeneo mengine yenye miti kila mahali pa dunia isipokuwa Madagaska, Australia, New Zealand na kanda za Aktiki na Antaktiki.

Spishi nyingi ni nyeusi mgongoni kwenye madoa na/au mabaka meupe au njano. Spishi nyingine zina rangi ya majani au kahawa. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Mkia una manyoya shupavu na umsaidia ndege kutembea wima mashinani kwa miti. Ndege hawa wana domo lenye nguvu ambalo hutumia kugogota miti na kutafuta wadudu katika nyufa za miti. Ulimi wao mrefu wa kunata na wenye nywele uwasaidia kuwatoa wadudu. Zaidi ya wadudu vigong'ota hula matunda na makokwa; spishi nyingine hula hata utomvu wa miti. Dume huchimba tundu katika mti na pengine jike amsaidia. Huyu huyataga mayai 2-6 ndani ya tundu.

Spishi za Afrika

Jenasi za mabara mengine

Picha

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!