Kamusi ya Tiba (KyT) ni kamusi iliyotolewa na TUKI inayokusanya istilahi za tiba. Inapanga istilahi kwa lugha ya Kiingereza na kuonyesha visawe vyake vya Kiswahili.
Kamusi hii iliandaliwa na wanaistilahi wawili wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni A.M.A. Mwita pamoja na H.J.M. Mwansoko na kuchapishwa mara ya kwanza mwaka 2003 kwa kutumia ISBN 9976-911-65-3.
Kamusi hii haipatikani kwa urahisi kwenye maduka ya vitabu nje ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hivyo istilahi zake hazikutumiwa katika makala za kwanza za tiba zilizotungwa katika wikipedia hii.