Hasira ni ono linalowapata binadamu na wanyama mbele ya kipingamizi.
Katika hali hiyo mtu hughadhibika, hata kuchukia kwa kupatwa na kitu ambacho yeye mwenyewe hapendi.
Mtu mwenye hasira ya mara kwa mara, hushauriwa ajaribu kuepuka mambo au vitu vinavyomuudhi, kwa mfano, anaweza kuondoka mahali penye maudhi, na kama ni kubishana aweze kunyamaza ili kuepukana na ugomvi.
Pia inashauriwa kuwa, kama unajua mwenzio hukasirishwa na kitu fulani, bora usimchokoze, kwa sababu ni hatari kwa maisha yako maana kwa hasira yake anaweza kufanya kitu chochote kibaya.
Isiporatibiwa na mhusika inaweza ikasababisha madhara makubwa, inavyofundisha mithali ya Kiswahili, "Hasira, hasara". Hasira hupelekea mtu kuvunja sheria kwa kujichukulia hatua mkononi na mwishowe kufanya jambo la hatari.