Fat Joe

Fat Joe
Fat Joe mnamo Aprili 2011
Fat Joe mnamo Aprili 2011
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Joseph Cartagena
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapper
Miaka ya kazi 1991 - hadi leo
Studio Relativity, Atlantic, Terror Squad, Imperial
Ame/Wameshirikiana na Terror Squad, D.I.T.C., Big Pun, DJ Khaled, The Game, Jadakiss, R. Kelly, KRS-One, Lil Wayne, Plies, Rick Ross
Tovuti Fat-Joe.com

Joseph Antonio Cartagena (amezaliwa 19 Agosti, 1970) ni rapa wa Kimarekani mwenyewe asili ya Puerto Rico na Kikuba. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Fat Joe. Fat Joe amesaini mkataba wa kurekodi na studio ya Imperial Records.

Fat Joe pia anaendesha studio yake mwenyewe iitwayo Terror Squad Entertainment, ambapo huko ndiyo mmiliki na ndiyo msanii mkubwa katika studio hiyo na pia kuwa kama mwimbaji kiongozi wa kundi lake la muziki la Terror Squad, ambalo limeshehena baadhi ya wasanii wengine rap wa mjini New York.

Albamu ya kwanza ya Fat Joe ilikuwa inaitwa Represent, ilitoka mnamo mwaka wa 1993, ikafuatiwa na Jealous One's Envy ya mwaka wa 1995. Kutoka mwaka wa 1998 hadi 2006, alisaini mkataba na studio ya Atlantic Records, na akafanikiwa kutoa albamu nne akiwa katika studio hiyo. Albamu hizo ni kama vile Don Cartagena (1998), Jealous Ones Still Envy (J.O.S.E.) kunako mwaka wa 2001, Loyalty (2002) na All or Nothing ya mwaka wa 2005.[1]

Baada ya kutoa albamu yake ya All or Nothing, Fat Joe akawa amejiingiza katika ugomvi mkubwa kabisa na msanii mwingine wa rap wa New York Bw. 50 Cent, ambaye alimshambulia Fat Joe katika nyimbo yake ya "Piggy Bank.

Muziki

Albamu za peke yake

Albamu za ushirika

Akiwa na D.I.T.C.

Akiwa na Terror Squad

Baadhi ya filamu

  • Thicker Than Water (1999) - Lonzo Medina
  • Prison Song (2001)
  • Empire (2002)
  • Scary Movie 3 (2003)
  • Happy Feet (2006) - sauti ya Seymour

Marejeo

  1. Prato, Greg (2008). "Fat Joe - Biography". All Music Guide. Iliwekwa mnamo 2008-04-18.
  2. Terror Squad Sign New Deal With Koch Records Ilihifadhiwa 5 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.. Boombox.co.uk: 23 Oktoba 2007

Viungo vya nje

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!