Diego Armando Maradona (amezaliwa 30 Oktoba 1960 - 25 Novemba 2020) alikuwa mchezaji maarufu wa mpira wa miguu kutoka nchi ya Argentina. Watu wengi wanamchukulia kuwa ni mchezaji bora duniani kwa wakati wote.
Mwaka 2000 katika zawadi ya mchezaji bora wa karne iliyotangazwa na FIFA, Maradona alikwenda sambamba katika kugombea mchezaji bora wa karne na Pele baada ya wote kuwa wa kwanza katika uchaguzi ambao FIFA ilitangaza kupitia rai za watu kwenye internet ili kuchagua mchezaji bora wa karne ya 20.
Maradona alichezea vilabu vya Boca Juniors, FC Barcelona na SSC Napoli na alipata tuzo mbalimbali katika vilabu hivyo vyote.