DaxibotulinumtoxinA, inayouzwa kwa jina la chapa Daxxify, ni dawa inayotumika kuboresha mwonekano wa mikunjo inayopatikana kati ya nyusi. [1] Inaweza pia kutolewa kwa ajili ya kutibu ugonjwa sugu wa neva unaosababisha shingo kugeukia kushoto, kulia, juu, na/au chini bila hiari (cervical dystonia).[2] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudunga sindano kwenye misuli.[1] Madhara yake yanaweza kudumu kwa hadi miezi sita.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuanguka kwa kope na shida ya kusonga uso.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya kumeza au kupumua.[1] Ni sumu ya botulinamu A (botulinum toxin A) ambayo huzuia kutolewa kwa asetilikolini (acetylcholine) na ni ajenti ya kuzuia neva za fahamu (neuromuscular blocking agent).[1]
DaxibotulinumtoxinA iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2022.[1] Ni mshindani wa kibiashara kwa Botox.[3]
Marejeo
|
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu DaxibotulinumtoxinA kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|