Dandora

Dandora ni mtaa ulio mashariki mwa Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Ni sehemu ya tarafa ya Embakasi.

Dandora ilianzishwa mwaka wa 1977, kwa mchango wa fedha kiasi kutoka kwa Benki ya Dunia ili kutoa makazi ya hali ya juu [1] Ilihifadhiwa 10 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. Hata hivyo, mtaa huu umegeuka na kuwa duni na wenye uhaba mkubwa wa ajira. Biwi la Nairobi la kutupa taka liko Dandora, na pengine husababisha matatizo ya afya kwa wakazi wa mtaa huu.

Mabwawa ya oksijeni ya Dandora, vipengele maarufu kwenye picha za satelaiti za eneo hilo, ndio eneo kuu la Nairobi la kusafisha maji taka na hufululiza maji yake katika Mto Nairobi.[1]

Dandora iliorodheshwa na Taasisi ya Blacksmith kama moja ya maeneo yenye uchafu mwingi zaidi duniani.[2]

Hivi majuzi, vikundi vingi vya muziki wa aina ya hip hop ya Kikenya vimeibuka kutoka Dandora, kwa mfano Kalamashaka. Utamaduni wa Hip Hop umeendeleza na kuchukua jukumu muhimu katika mtaa wa Dandora hivi kwamba wasanii wengi wameamua kutumia hip hop kama nguvu za kijamii zenye mwelekeo bora. Ziara ya hivi majuzi ya kundi la wasanii wa hip hop la Marekani Dead Prez kumeongezea kutazamwa kwa makini hali ya umaskini wa Dandora. "Hip-hop ni chombo chenye nguvu tunachoweza kutumia kuelimisha wale walio katika giza hivyo kama msanii akinyanyua kipaza sauti na kuroga kuhusu utajiri na vifaa vya urembo wakati jamii yake ni maskini sana basi yeye anawadanganya watu kwa sababu kile anachoimba kuhusu si kweli. Jamii zetu ni maskini hatuna chochote hivyo basi kwa nini tuimbe kuhusu mambo ambayo si hatuna. Makampuni makubwa yanatohadaa hivyo hatupaswi kuanguka katika mtego wao kwa urahisi, "alielezea mwanachama wa Dead Prez wakati wa ziara yao. Hatimaye Dandora imeanza kupata kasi katika kupata makini kwa masuala ya kibinadamu na mazingira katika makazi hayo duni[3]

Marejeo

  1. BirdLife IBA Factsheet
  2. "World's Worst Polluted Places 2007". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-26. Iliwekwa mnamo 2010-01-11.
  3. http://www.africanhiphop.com/index.php?module=subjects&func=viewpage&pageid=281

1°15′S 36°54′E / 1.250°S 36.900°E / -1.250; 36.900

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!