Adiós Sabata (Kiitalia: Indio Black, sai che ti dico: Sei un gran figlio di ..., kwa tafsri ya haraka unaweza sema "Indio Black, unajua ni nini nitakacho kwambia wewe... Wewe ni mtoto mkubwa wa ....") ni filamu ya Spaghetti Western iliyotolewa mwaka 1971 na iliongozwa na bwana Gianfranco Parolini.
Hapo awali filamu ilibidi iyende kwa jina la Indio Black, lakini jina lilibadilishwa kutokana kwamba filamu ya kwanza ilifanya vizuri kwa jina la Sabata na ikaonekana kuwa na wapenzi wengi kuliko. Filamu hii ilibdi acheze Lee Van Cleef, lakini Cleef hakucheza kwasababu alikuwa anacheza filamu ya The Magnificent Seven Ride, humo alitumia jina lile lile la Chris Adams, ambalo Brynner alibebea umaarufu katika filamu ya awali ya The Magnificent Seven.
Njama
Muhtsari wa filmu
Ilikuwa ndani ya nchi Mexiko iliyokuwa chini Dola la Maximilian I, Sabata alikodiwa na kiongozi wa guerilla bwana Señor Ocaño kwenda kuiba wagonload (Farasi mwenye kijumba nyuma) wa dhahabu kutoka mikononi mwa majeshi ya Kiaustrian. Sabata na rafiki zake wawili Escudo na Ballantine walifanikiwa kulitwaa wagon, lakini hawakukuta dhahabu bali waliukuta mchanga katika wagon hiyo, na dhabu ilikuwa ishachukuliwa na Amiri jeshi mkuu wa Kiaustria bwana Skimmel. Kwa hiyo Sabata akapanga mpango wa kurudisha dhahabu hizo.